Mitindo

Jinsi ya kunyoa ndevu kwa raha

Tarehe January 9, 2017

shavingguy-shutterstock

Moja  ya matatizo makubwa kwa wanaume ni unyoaji wa ndevu, kitu ambacho
wakati mwingine huwakera wahusika na wao kujiona kama ni wafungwa.

Ndevu huwafanya wanaume wengi kuhisi kuwa ni tatizo kubwa sana kwao kwani wakati wa kuzinyoa huwa ni tatizo kubwa kutokana na wengine kuweza kupata matatizo wakati wa kunyoa ndevu.

Ili kuondoa matatizo haya yafuatayo yanaweza kabisa kukusaidia kukuweka katika
aina Fulani ya raha kubwa.

Chagua mashine ya kunyolea na wembe ambao unadhani unaswihi ngozi
yako, kuna aina nyingi sana za mashine za kunyolea pamoja na nyembe
zake ni muhimu kujua wembe ambao unatumia kwa kuzingatia mahitaji yako
hasa ya aina ya ndevu.

Weka uso safi na usio mchafu, Safisha kabla ya kunyoa, hii
inakusaidia kufungua matundu yanayoshikilia ndevu kabla ya kunyoa ili
kuweza kupata mnyoo laini na wenye uhakika.

Usisahau kuloweka kidevu chako vyema, hii inasaidia wenye kupita
kiulaini zaidi na kama unatumia kiwembe cha kawaida basi ni vyema sana
kufanya kazi hiyo ukitoka kuoga.

Tumia maji ya moto siyo yanayounguza kama inawezekana, yanasaidia
sana kufungua vishimo vya vinyweleo, pia unaweza kupata masaji ya
chapchap katika uso ili kusaidia kulainisha kidevu chako.

Chagua krimu hasa inayostahili kwako ya kunyolea kwa kutegemea ngozi
yako na chagua linalostahili unalotaka,  jipake kiasi cha kutosha
katika sehemu zinazostahili kwani husaidia kuburudisha ngozi.

Baada ya kujinyoa, osha uso wako na ondoa krimu zote,tumia
moistrurizer baada ya kunyoa.
 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni