Mitindo

Faida ya manjano kwenye urembo

Tarehe December 19, 2016

 

images-2

Siku hizi mambo yamebadilika manjano yamekuwa ni kiungo muhimu katika ngozi, wakati hapo awali manjono yalikuwa yanatumika katika kupikia, lakini kwa sasa katika urembo bila manjano urembo wako unakuwa haujakamilika kabisa, manjano mbichi haijazimuliwa na sembe ndio nzuri, maana unaweza ukanunua manjano yakawa teyari  yashachanganywa na sembe.

Manjano yanaweza kukusaidia katika urembo kama ifuatavyo;

Kutibu chunusi, Kutokana na tabia yake ya kupambana na bakteria manjano inauwezo wa kukausha chunusi hasa zile zinazotokana na maambukizi ya bakteria,  kwa wenye ngozi ya mafuta unachanganya manjano na  maji ya waridi na wale wenye ngozi kavu unachanganya manjano  na maziwa fresh kisha unapaka usoni kwa nusu saa kisha unaosha na  maji ya kawaida.

Pia manjano Inang’arisha ngozi, Manjano inatabia ya kutoa weusi kwenye ngozi unaotokana na cream,kuungua jua au kufubaa kwa ngozi, unatakiwa uchanganye manjano na maji ya waridi kisha sugua sehemu iliyoathirika.

Manjano  Inapunguza mafuta  Kwa wenye ngozi ya mafuta  pia manjano inasaidia sana kupunguza uzalishaji wa mafuta,hapa mtashanga kidogo, Unakunywa  glasi  moja ya mchanganyiko wa maji na manjano angalau mara  mbili kwa wiki, Pia unaweza kuchanganya manjano,limao na maji ya waridi na kupaka usoni kwa dakika 30.

Manjano inasaidia kupunguza kasi ya ngozi kuzeeka  baada ya matumizi ya make up wiki nzima jitahidi mwisho wa wiki uwe unafanya facial ya manjano angalau mara moja,maana manjano husaidia ngozi isichoke haraka na hivyo kupaka mwonekano mzuri wa ngozi yako.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni