Michezo/Sports

Young Africans, Simba SC ngoma droo

Tarehe October 28, 2017

Kiungo mkabaji wa Young Africans Papy Tshishimbi alikuwa muhimu kwenye mchezo wa Oktoba 28 kwa namna alivyovuruga mipango muhimu ya Simba SC.

SHIZZA KICHUYA, OBREY CHIRWA WAFANYA KWELI

Kwa ulimwengu wa kandanda kubeti ndio imekuwa sehemu ya maisha ya watu ya kila siku. Haijalishi ni mechi kubwa au ndogo.

Inapotokea mechi kubwa kila kichochoro hususani maeneo ya mijini hubana kwa watu kutembea na peni na karatasi ukidhani wanasoma mahesabu. Oktoba 28 mwaa huu kabla ya mechi ya Ligi Kuu Tanzania Bara baina ya watani wa jadi wa Kariakoo, Dar es Salaam kulikuwa na makundi ya watu wengi wakibeti mchezo huo.

Mashabiki wa Young Africans walibeti ushindi wa timu yao huku wale wa Simba nao wakifanya hivyo hivyo. Kilichotokea leo katika Uwanja wa Uhuru ni ngoma droo baina ya miamba hiyo ya kandanda nchini.

FT: YOUNG AFRICANS 1-1 SIMBA SC

Bao la Simba lilifungwa katika dakika ya 57 baada ya kazi nzuri ya Emmanuel Okwi aliyepiga mpira uliiokolewa na mlinda mlango wa Young Africans Youthe Rothestand. Dakika tatu baadaye Young Africans walisawazisha kupitia kwa raia Zambia Obrey Chirwa akimalizia mpira uliopigwa na Geoffrey Mwashiuya na kumtungua Mlinda mlango wa Aishi Manula.

Katika mchezo huo Juuko Murshid wa Simba alikula sahani moja na Ibrahim Ajibu kama Andrew Vincent ‘Dante’ alipokuwa akitembea hatua kwa hatua na Okwi. Pia Papy Tshishimbi alionekana mwiba kwa mipira michache mirefu aliyothubutu kujaribu kupiga katika lango la Simba SC.

KIKOSI CHA YANGA SC

Youthe Rostand, Juma Abdul, Gadiel Michael, Andrew Vincent ‘Dante’, Kelvin Yondani, Papy Kabamba Tshitshimbi, Pius Buswita, Raphael Daudi/Pato Ngonyani dk 65, Obrey Chirwa, Ibrahim Ajib na Geoffrey Mwashiuya.

KIKOSI CHA SIMBA SC

Aishi Manula, Erasto Nyoni, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Juuko Murshid, Method Mwanjali, James Kotei/Jonas Mkude dk 75, Shiza Kichuya, Muzamil Yassin/Said Ndemla dk 84, Emmanuel Okwi, Laudit Mavugo/John Bocco dk 75 na Haruna Niyonzima.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni