Michezo/Sports

Yissa awatisha Ngoma, Tambwe

Tarehe August 10, 2017

Kehinde Yissa Anifowoshe katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Agosti 10, 2017.

Kehinde Yissa Anifowoshe katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Agosti 10, 2017.

Mchezaji mpya wa klabu ya Yanga Kehinde Yissa Anifowoshe amefanya mazoezi na kikosi cha kocha Geroge Lwandamina katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam huku ikishuhudiwa uwezo wake wa kumiliki mpira kuwazuia washambuliaji mahiri wa klabu hiyo.

Washambuliaji raia wa Zimbambwe Donald Ngoma na raia wa Burundi Amissi Tambwe wameukubali muziki wa raia huyo wa Nigeria aliyetokea Oman katika klabu ya Ittihad kutokana na uwezo wake wa kuharibu mipango yao. Pia washambuliaji hao wamepongeza namna anavyoweza kuipanga safu yake ya ushambuliaji.

Ilikuwa hivi mapema asubuhi ya Agosti 10 walitinga katika Uwanja wa Uhuru ambako Lwandamina alianza na mazoezi mepesi na baadaye mazoezi ya kupiga pasi na namna ya kujipanga. Yissa alionyesha uwezo mkubwa wa upigaji wa pasi kama haitoshi namna anavyojiposition iliwavutia sana watazamaji wa mazoezi hayo.

Kocha Lwandamina alikuwa akiwafanyisha mazoezi ya 10vs8 ambayo kila wakati Yissa aliangukia katika kikosi cha wachezaji wanane huku Ngoma na Tambwe wakiwa katika kikosi cha wachezaji 10. Dakika 25 za mazoezi hayo ya namna ya kushambulia na kuzuia  mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya MFM aliweza kufanya makubwa kwa kufanya blocks za kutosha pindi kina Thabani  Kamusoko na wenzake walipotaka kupitisha mipira.

Hata hivyo Yissa anasema amevutia na kikosi cha Yanga ambacho amefanya nacho mazoezi na kusema sio wabaya atadumu kucheza nao.

Aidha umahiri wa mlinzi huyo wa kati ni salamu tosha kwa mahasimu wao Simba ambao nao katika kipindi cha usajili wamesajili kwa kufuru Emmanuel Okwi, Haruna Niyonzima, John Bocco, Ali Shomari na wengineo.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni