Michezo/Sports

Yanga yalamba mkataba mnono na kampuni ya Macron

Tarehe January 17, 2018

Klabu ya Yanga kutoka Jangwani jijini Dar es salaam wamesaini mkataba wa miaka 3 na kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya michezo Macron wenye thamani ya bilioni mbili.

Mkurugenzi mtendaji wa kampuni hiyo nchini Tanzania Suleiman Karim amewahakikishia wana Yanga kuwa klabu hiyo itapata faida kupitia mauzo ya jezi orijino za klabu yao.

Katika mkataba huo uliosainiwa kwenye makao makuu ya klabu hiyo, Yanga itatoa haki zote za utengenezaji na usambazaji wa jezi zao huku pia nembo ya kampuni ya Macron itaanza kuonekana kwenye jezi za Yanga SC.

Kwa upande wake Katibu mkuu wa Yanga Charles Mkwasa amewaonya wote wanaouza jezi za klabu hiyo bila kuwepo kwa makubaliano na watawachukulia hatua za kisheria kwasababu sasa yupo mwenye haki ya kufanya hivyo.

Kampuni ya Macron inafanya kazi katika nchi zaidi ya 16 duniani zikiwemo England, Italia na Ufaransa. Hivi karibuni kampuni hiyo iliingia mkatata wa miaka 2 na timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) wenye thamani ya milion 800.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni