Michezo/Sports

Yanga ‘out’ Mapinduzi Cup kwa mikwaju ya penati

Tarehe January 10, 2017

Picha-Simba1

Timu ya Simba leo imefanikiwa kutinga fainali ya michuano ya kombe la Mapinduzi baada ya kuwachabanga watani wao, Yanga goli 4-2.

Wababe hao walitoshana nguvu ya bila kufungana hadi dakika 90 za mchezo zinamalizika na hivyo kulazimika kupigiana mikwaju ya penati na Simba kuibuka kidedea kwa goli 4-2.

Sasa fainali ya kombe la mapinduzi itakuwa kati ya Azam FC na Simba SC baada ya leo mapema Azam kuibamiza Taifa Jang’ombe kwa goli 1-0.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni