Michezo/Sports

Yanga kuwakabili Ruvu Shooting

Tarehe August 10, 2017

Kikosi cha Yanga

Kikosi cha Yanga

Kikosi cha timu ya Yanga kinatarajia kushuka dimbani Agosti 12 kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya Ruvu Shooting ya mkoani Pwani.

Mchezo huo unaotarajiwa kupigwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam,unatarajiwa kuwa na ushindani wa hali ya juu kutokana na timu hizo kuwa kwenye maandalizi ya kujiwinda na msimu ujao wa ligi kuu ya Tanzania bara.

Mbali na mchezo huo utakaopigwa siku ya jumamosi pia kikosi cha Yanga kinatarajiwa kucheza mechi nyingine ya kirafiki na timu ya Mlandege FC ya Zanzibar, mechi itakayochezwa siku inayofuata kwenye uwanja wa  Amani huko Zanzibar.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni