Michezo/Sports

Welbeck: Chamberlain anafaa kucheza kiungo wa kati

Tarehe June 16, 2017

Alex Oxlade Chamberlain

Alex Oxlade Chamberlain

Danny Welbeck amemtamkia waziwazi mchezaji mwenzake wa klabu ya Arsenal Alex Oxlade Chamberlain kuwa ni mzuri kwa kuwa kiungo wa kati.

Nyota huyo mwenye miaka 23 amekuwa akitumiwa na kocha Arsene Wenger katika maeneo tofauti ndani ya uwanja tangu alipojiunga na Washika bunduki hao wa Kaskazini mwa London akitokea Southampton mwaka 2011.

Mkondo wa pili wa msimu uliopita Chamberlain alihudumu katika nafasi ya winga kwenye kikosi cha Arsenal. Welbeck ambaye alijiunga klabuni hapo akitokea Manchester United amesema nyota huyo wa zamani wa Portsmouth anafaa zaidi akicheza katika nafasi ya kiungo wa kati.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni