Michezo/Sports

Umeisikia kauli ya Mexime dhidi ya Young Africans?

Tarehe October 12, 2017

INFOGRAPHIC: Kocha wa Kagera Sugar Meck Mexime akizungumza kuelekea mchezo wake dhidi ya Young Africans Oktoba 14 mwaka huu.

 “Hata kama nitafungwa na Yanga Jumamosi siwezi kuachia ngazi, kwani kufanya hivyo ni sawa na kuwaacha wachezaji wangu kwenye mataa. Yanga ni timu kubwa yenye uwezo wa kuifunga timu yoyote lakini sisi (Kagera Sugar) tunaweza kuzindukia kwao.”

Mecky Mexime, Oktoba 2017

Kagera Sugar imekuwa kwenye wakati mgumu tangu kuanza kwa msimu huu wa 2017/18, ikiwa haijaonza ushindi hata mechi moja kati ya mechi tano ilizocheza , ikifungwa mara tatu na kuambulia sare mbili hivyo kujikuta ikiburuza mkia katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu ikiwa na alama mbili tu.

Mexime aliwahi kuwa nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania na Mtibwa Sugar. Wikiendi hii Kagera Sugar inaikaribisha Young Africans katika dimba la Kaitaba mjini Bukoba ikiwa ni mzunguko wa sita.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni