Michezo/Sports

Tuhuma za kukwepa kodi huenda zikamng’oa Ronaldo Madrid

Tarehe June 17, 2017

Christiano Ronaldo akishangilia na wachezaji wenzake

Christiano Ronaldo akishangilia na wachezaji wenzake

Mchezaji wa Klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania, Cristiano Ronaldo huenda akafanya maamuzi magumu na kuihama klabu hiyo naada ya kuonekana kukerekwa na tuhuma za udanganyifu wa ulipaji kodi zinazoendelea nchini Hispania.

Mtu wa karibu wa mchezaji huyo ameliambia shirika la habari la BBC kuwa Ronaldo anafikiria kuondoka Madrid.

Ronaldo, aliyejiunga na Real Madrid akitokea Manchester United mwaka 2009 kwa dau la paundi milioni 80, mkataba wake unafikia euro bilioni moja (£874.88m).

Ligi ya China tayari imeonyesha nia ya kuhitaji huduma ya Mreno huyo lakini washauri wake wakaribu wanapenda achezee Ulaya ama kwenda kukipiga katika klabu ya Paris St-Germain ya Ufaransa.

Ronaldo, ameisadia Real kushinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mara tatu na La Liga mara mbili, anatuhuma za udanyafu wa ulipajikodi wa takribani euro 14.7m (£13m; $16m) kati ya mwaka 2011 na 2014.

Hasimu wake mkubwa, Lionel Messi wa Barcelona naye amekutwa na hatia ya kukwepa kodi hivi karibuni na kuhukumiwa kifungo cha jela lakini akalipa faini na kukimbia jela.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni