Michezo/Sports

Tetesi za Soka Ulaya leo Jumatatu

Tarehe November 13, 2017

Lionel Messi.

Hizi ni tetesi za soka la ulaya  siku ya leo jumatatu,

Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi ameitaka klabu hiyo kumtafuta mchezaji wa kiungo cha kati wa Tottenham Dele Alli, 21, kabla ya Real Madrid hawajafanya hivyo. (Don Balon – in Spanish)

Mshambuliaji wa Atletico Madrid Fernando Torres, 33, ana nia ya kurejea Premier League huku Southampton na Newcastle wakitaka kumsaini. (Daily Mirror)

Manchester United wako tayari kulipa pauni milioni 177 kumsaini mchezaji wa kati wa Real Madrid Marco Asensio, 21. (Don Balon – in Spanish)

Manchester United wanataka kumuuza mchezaji wa England Luke Shaw ,22, kwa karibu pauni milioni 20 mwezi Januari. (Times – subscription required)

Patrice Evra amezungumza na vilabu kadha vinavyotaka kumsaini licha ya kumvamia shabiki wa Marseille kwa mujibu wa ajenti wake. (Gazzetta dello Sport – in Italian)

LiverpooL wanataka kutumia paunia milioni 5 kumsaini mchezaji wa miaka 17 wa Wolves Morgan Gibbs-White mwezi Januari. (Sun)

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni