Michezo/Sports

Tanzania yashuka viwango FIFA, Brazil yarudi

Tarehe August 10, 2017

Coutinho, Neymar na Gabriel Jesus.

Coutinho, Neymar na Gabriel Jesus.

Tanzania imeshuka nafasi sita katika viwango vya soka vinavyotolewa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), ikishika nafasi ya 121.

Katika ukanda wa Afrika Mashariki bado Uganda inaendelea kuongoza ikiwa katika nafasi ya kwanza kwa Afrika Mashariki ikishika nafasi ya 73 ikipanda nafasi moja mwezi huu, huku Kenya ikishika nafasi ya 82 ikipanda nafasi mbili.

Katika Top 10 ya dunia, Ujerumani imeshushwa na Brazil imerudi katika nafasi ya kwanza baada ya mwezi mmoja wa kuwa chini. Argentina imeendelea kushika nafasi ya tatu. Uswisi imepanda nafasi moja ikishika nafasi ya nne. Poland (5), Ureno (6), Chile(7), Colombia(8), Ubelgiji (9) na Ufaransa (10).

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni