Michezo/Sports

Sare yaiponza Twiga Stars,yatupwa nje AFCON

Tarehe April 9, 2018

taifa ya soka ya wanawake Twiga Stars.

Hatimaye,timu ya taifa ya soka ya wanawake Twiga Stars imetupwa nje ya mashindano ya kuwania kufuzu fainali za AFCON 2018.

Twiga Stars imetolewa  baada kutoa sare ya 1-1 ugenini dhidi ya Zambia licha ya kujitahidi kuzuia kufungwa.

Twiga stars imeponzwa na  sare ya 3-3 ambayo ilipatikana kwenye mchezo wa kwanza uliopigwa kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Jumanne iliyopita.

Baada ya Twiga Stars kutolewa Zambia sasa imesonga mbele ambapo imebakiza mchezo mmoja.

Zambia  itacheza na mshindi kati ya Namibia na Zimbabwe na endapo itashinda basi itakuwa imekata tiketi ya kucheza fainali hizo zitakazofanyika nchini Ghana.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni