Michezo/Sports

Sanchez kuukosa ufunguzi PL Agosti 11

Tarehe August 10, 2017

Alexis Sanchez

Alexis Sanchez

Kocha Arsene Wenger ameweka bayana kuwa atamkosa nyota wake raia wa Chile Alexis Sanchez katika mchezo wa kufungua msimu wa Ligi Kuu ya England (PL) dhidi ya Leicster City.

Wenger alisema, “Sanchez hatkuwapo, ana maumivu kidogo ya tumbo aliyoyapata asubuhi ya Jumamosi tukiwa mazoezi kabla ya kwenda Wembley. Yupo nje kwa muda, sijui atakuwa nje kwa muda gani wiki mbili au wiki moja. Pia hatacheza dhid ya Stoke.”

Katika mechi sita zilizopita Arsenal imetoka sare mbili, ikipoteza mbili na kushinda tatu huku Leicester ikitoka sare moja ikipoteza tatu na kushinda mbili. Arsenal ilipoteza dhidi ya Sevilla na Chelsea, ikitoka sare na Bayern Munich na Chelsea katika muda wa kawaida, ilishinda dhidi ya Western Sydney Wanderers na Benfica.

Leicester City ilipoteza dhidi ya Burton Albion, Wolverhampton na Liverpool, ikashinda dhidi ya Borussia Moenchengladbach na Luton, ilitoka sare na MK Dons

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni