Michezo/Sports

Samatta asaini mkataba kuwanoa vijana

Tarehe June 19, 2017

Genk's Spanish midfielder Alejandro Pozu

Nahodha wa Timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ na mshambuliaji wa KRC Genk ya Ubeligiji, Mbwana Samatta ameingia mkataba maalumu na Benki ya DTB  ambapo pamoja na mambo mengine, ataendesha kliniki ya soka kwa mamia ya vijana.

Akizungumzia mkataba huo, Samatta amesema una lenga kuhamasisha vijana ili kuendeleza soka la Tanzania.

“Nitakuwa balozi wa DTB (Diamond Trust Bank), nikifanya kazi mbalimbali za kijamii na masuala ya kimichezo,” amesema Samatta muda mfupi baada ya kumaliza kutoa mafunzo ya soka jana katika viwanja vya Kituo cha Michezo cha Jakaya Kikwete, Kidongo Chekundu, Jijini Dar es Salaam.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni