Michezo/Sports

Rais TFF apata shavu fainali za CHAN

Tarehe January 13, 2018

Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF limemteua Rais wa shirikisho la soka nchini TFF Wallace Karia kuwa kamishna wa mechi ya ufunguzi wa fainali za ndani (CHAN) kati ya wenyeji Morocco dhidi ya Mauritania itakayochezwa kesho Januari 13.

Michuano hiyo ambayo inafanyika kwa mara ya tano tangu ianzishwe, inatarajiwa kuanza kesho ikishirikisha nchi 16 na itamalizika Februari 4, 2018 nchini Morocco.

Kabla ya Morocco kupewa uenyeji wa michuano hiyo awali ilikuwa ifanyike nchini Kenya ambapo shirikisho la soka Afrika CAF lilibadilisha kutokana na Kenya kushindwa kumaliza maandalizi ndani ya wakati.

Katika michuano hiyo Rwanda iliifungashia virago Tanzania baada ya kutoka sare kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa CCM Kirumba.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni