Michezo/Sports

Rais FIFA uso kwa uso na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa

Tarehe February 23, 2018

Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) Gianni Infantino.

Rais wa Shirikisho la Soka la duniani (FIFA) Gianni Infantino, amewasili nchini Tanzania kuhudhuria mkutano wa shirikisho hilo nchini.

Mkutano huo ulishirikisha jumla ya mashirikisho 21 ya kandanda ambao ni wanachama wa shirikisho hilo.

Rais wa shirikisho hilo la soka duniani alikutana na Waziri Mkuu wa nchi , Kassim Majaliwa pamoja na Waziri wa Utamaduni na Michezo Harryson Mwakyembe.

Katika mkutano na waandishi wa habari, Bw Infantino amesisitiza kuzungumzia hali ya rushwa katika mpira wa miguu

Akizungumzia jitihada za kukuza soka barani Afrika, Bw Infantino ameelezea kuwa siku za nyuma Afrika ilikuwa inapata dola za kimarekani milioni 26 kutoka FIFA, lakini sasa hivi, Afrika inapata dola za kimarekani milioni 100 ili kuiinua mchezo wa soka.

Pamoja na hayo amesema katika kipindi chake amejaribu kuhakikisha ongezeko la timu za Afrika katika kushiriki michuano ya kombe la dunia .

Tangu aingie madarakani ,Rais huyo wa Fifa ameongeza idadi ya timu zitazoshiriki michuano ya kombe la dunia la mwaka 2026 toka 5 mpaka 7.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni