Michezo/Sports

Nyosso ampiga ngumi na kuzimia shabiki wa Simba

Tarehe January 23, 2018

Mlinzi wa Kagera Sugar Juma Said Nyosso amekamatwa na Askari wa Jeshi la Polisi Mkoani Kagera kufuatia kumpiga shabiki wa Simba baada ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Simba uliopigwa mjini Bukoba.

Inadaiwa kuwa baada ya mechi kumalizika na wachezaji wa Kagera Sugar walikuwa wanakwenda katika vyumba vya kubadilishia nguo na mashabiki wakawa wanashangilia kwa kutoa maneno makali kitendo ambacho kilimfanya Nyosso akose uvumilivu na kumpiga shabiki huyo.

Shabiki huyo baada ya kipigo alianguka chini na kupoteza fahamu ndipo  Polisi walifika na kumkamata Nyosso na kuondoka naye kwenda kituo cha Polisi mkoani humo.

Mlinzi wa Kagera Sugar Juma Said Nyosso akiwa mikononi mwa Polisi.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni