Michezo/Sports

Ndikumana wa Uwoya afariki dunia

Tarehe November 15, 2017

Mume wa zamani wa Muigizaji, Irene Uwoya, Ndikumana Hamadi amefariki dunia ghafla Jijini Kigali, Rwanda.

Habari za awali zimethibitisha kifo cha mwanasoka huyo ambaye amezaa mtoto mmoja na Irene.

Ndikumana maarufu kama ‘Katauti’ aliyewahi kuichezea Klabu ya Stand United, kwa sasa alikuwa kocha msaidizi wa timu ya soka ya Rayon Sports ambayo inaongoza kwa kuwa na mashabiki wengi nchini Rwanda.

Uongozi wa timu hiyo umesema kuwa jana Katauti alifanya mazoezi na wachezaji wake akiwa buheri wa afya lakini baadae mwili wake ulikutwa nyumbani kwake Mjini Kigali akiwa amefariki dunia huku ugonjwa wa moyo ukitajwa kuwa ndi sababu iliyopelekea kifo chake.

“Alisikia maumivu makali kifuani akaomba soda ya baridi wakamletea na alipomaliza kunywa tu kidogo akatapika na akaishiwa pumzi na ndipo akakata kauli, bado tunasubiri uchunguzi wa kina wa kitabibu,” umesema uongozi huo.

Kwa siku za hivi karibuni Ndikumana alionekana akitumia mitandao ya kijamii kusema machache kuhusiana na aliyekuwa mke wake Irene Uwoya ambaye kwa sasa ameolewa na Mwanamuziki, Dogo Janja.

Siku chache baada ya kusambaa kwa picha za harusi za aliyekuwa mke wake, Irene Uwoya, kuonekana amefunga ndoa na Dogo Janja, Ndikumana alionekana kuumizwa na ndoa hiyo licha ya kuwa kwa sasa alikuwa na mpenzi mwingine na kuandika maneno mitandaoni na kupelekea mashabiki wake kudai kuwa anaumwa ‘homa ya wivu.’

Irene na Ndikumana walifunga ndoa mwaka 2009 na kufanikiwa kupata mtoto mmoja wa kiume waliyempa jina la Krish, lakini ndoa yao haikudumu kwa muda mrefu na kuamua kutengana.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni