Michezo/Sports

Nadal atolewa Nitto ATP

Tarehe November 14, 2017

Rafael Nadal

Usiku wa jana Jumatatu haukuwa mzuri kwa mchezaji mahiri wa tenisi Rafael Nadal baada ya kupoteza mechi hivyo kuashiria kuwa sherehe za mwaka huu za Christmas hazitafurahiwa vizuri. Nadal aliondolewa katika viwanja vya London O2 kutokana na majeruhi ya magoti.

Nyota huyo wa Hispania ameondoka baada yakutandikwa kwa seti 7-6, 6-7 6-4 na mchezaji wa Ubelgiji ambaye ni namba saba kwa ubora duniani David Goffin hivyo kumwaacha Roger Federer katika mbio za ubingwa huo. Hizo zilikuwa fainali zake za sita katika medani ya tenisi kwa Nadal mwenye miaka 31 ikiwa ni mwendelezo wa kufanya vibaya baada ya fainali zile za US Open.

Nadali alikaririwa akisema, “ Nilijua wakati wa mchezo.”  Nyota huyo alitolewa baada ya kipute cha saa 2:30 dimbani na Goffin.

David Goffin na Nadal baada ya mchezo jijini London.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni