Michezo/Sports

Mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu Juni 20

Tarehe June 19, 2017

Imani Madega miongoni mwa waliochukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais katika uchaguzi mkuu ujao wa Shirikisho la Soka Tanzania Bara (TFF).

Imani Madega miongoni mwa waliochukua fomu ya kuwania nafasi ya Urais katika uchaguzi mkuu ujao wa Shirikisho la Soka Tanzania Bara (TFF).

Wakati kesho Jumanne Juni 20, 2017 itakuwa mwisho wa kuchukua na kurejesha fomu kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), wagombea 62 tayari wamejitokeza.

Wanafamilia hao ni wale waliojitokeza kuanzia Ijumaa iliyopita Juni 16, mwaka huu wakiongozwa na Jamal Malinzi aliyekuwa wa kwanza kuchukua fimu kati ya wagombea tisa walioomba nafasi hiyo.

Fomu hizo zinachukuliwa na kurejeshwa katika ofisi za TTF, Karume jijini Dar es Salaam na Uchaguzi wa TFF utakafanyika Agosti 12, mwaka huu mkoani Dodoma.

Mbali ya Malinzi, wengine waliochukua fomu hizo ni Imani Madega, Wallace Karia, Fredrick Masolwa, Athumani Nyamlani, Fredrick Mwakalebela na Ally Mayay wakati waliojitokeza kuwania Makamu wa Rais wako Mulamu Nghambi, Michael Wambura, Geofrey Nyange, Mtemi Ramadhani na Robert Selasela.

Wajumbe wa Kamati ya Utendaji kwa kufuata Kanda 13 ni kama ifuatavyo:

Kanda Na. 1 Mikoa ya Kagera na Geita;

 1. Soloum Chama
 2. Kaliro Samson
 3. Samwel Daniel
 4. Leopold Mukebezi
 5. Abdallah Mussa

Kanda Na. 2 Mikoa ya Mara na Mwanza;

 1. Vedastus Lufano
 2. Ephraim Majinge

Kanda Na. 3 Mikoa ya Shinyanga na Simiyu;

 1. Benista Rugora
 2. Mbasha Matutu
 3. Stanslaus Nyongo

Kanda Na. 4 Mikoa ya Arusha na Manyara;

 1. Omari Walii
 2. Sarah Chao
 3. Peter Temu

Kanda Na. 5 Mikoa ya Kigoma na Tabora;

 1. John Kadutu
 2. Issa Bukuku
 3. Abubakar Zebo

Kanda Na. 6 Mikoa ya Katavi na Rukwa;

 1. Kenneth Pesambili
 2. Baraka Mazengo

Kanda Na. 7 Mikoa ya Mbeya na Iringa;

 1. Elias Mwanjala
 2. Cyprian Kuyava
 3. Erick Ambakisye

Kanda Na. 8 Mikoa ya Njombe na Ruvuma;

 1. James Mhagama
 2. Golden Sanga
 3. Vicent Majili

Kanda Na. 9 Lindi na Mtwara;

 1. Athuman Kambi
 2. Dunstan Mkundi

Kanda Na. 10 Mikoa ya Dodoma na Singida; 

 1. Hussein Mwamba
 2. Mohamed Aden
 3. Musa Sima
 4. Stewart Masima
 5. Ally Suru

Kanda Na. 11 Mikoa ya Pwani na Morogoro;

 1. Charles Mwakambaya
 2. Gabriel Makwawe
 3. Francis Ndulane

Kanda ya 12. Mikoa ya Kilimanjaro na Tanga

 1. Khalid Mohamed
 2. Goodluck Moshi

Kanda Na. 13 Mkoa wa Dar es Salaam

 1. Emmanuel Ashery
 2. Ayoub Nyenzi
 3. Saleh Alawi
 4. Shaffih Dauda
 5. Thabit Kandoro
 6. Abdul Sauko
 7. Peter Mhinzi
 8. Ally Kamtande
 9. Said Tully
 10. Mussa Kisoky
 11. Lameck Nyambaya
 12. Ramadhani Nassib
 13. Aziz Khalfan

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni