Michezo/Sports

Mo ashinda zabuni kuwekeza Simba kwa hisa

Tarehe December 3, 2017

Mohammed Dewji akisalimiana na mmoja wa wadau kwenye jukwaa kuu wakati wa tamasha la Simba Day.

Klabu ya Simba imemtangaza Mfanyabiashara na Mwanachama wake, Mohamed Dewji kuwa ndiye mshindi wa zabuni ya kuwekeza na kumiliki asilimia 49 ya hisa katika klabu hiyo kwa ofa ya Shilingi Bilioni 20.

Dewji ametangazwa mshindi katika mkutano uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere uliopo Posta.

Kwa hatua hiyo, Simba sasa inaingia rasmi katika mfumo wa uendeshwaji kwa njia ya hisa.

Bilionea Dewji alijitokeza na kuwa mwekezaji pekee ambaye aliweka dau la Shilingi bilioni 20 kupata hisa asilimia 51 lakini baada ya mchakato huo makubaliano yakawa ni hisa 49 anazoruhusiwa kuchukua kwa kitita hicho cha Shilingi Bilioni 20.

Mwenyekiti wa kamati ya mchakato huo zabuni, Jaji mstaafu Thomas Mihayo amesema, Mo Dewji amepita na kwamba kitachofuatia ni majadiliano mengine baada ya mkutano wa leo.

“Mohammed Dewji ndiye mshindi wa kuwania kuwekeza katika klabu ya Simba. Baada ya mkutano huu kutakuwa na majadiliano,” alisema.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni