Makala Maalumu

Mfahamu Lionel Messi ‘RECORD MAN’

Tarehe December 1, 2017

Lionel Messi

Baada ya Lionel Messi kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia Camp Nou, Barcelona ambao utakuwa ukimpa kiasi cha pauni 500,000 kwa wiki, tupitie rekodi mbalimbali za nyota huyo wa Argentina na mshindi wa tuzo ya Balon d’Or mara tano. Rekodi hizi ni kabla ya Novemba 25, 2017.

  1. Messi ameweka rekodi ya kuwa mfungaji bora wa La liga wa zama zote akifunga mabao 361 akimzidi Cristiano Ronaldo wa Real Madrid mwenye mabao 286 yakiwa ni mabao 75.
  2. Pia Muargentina huyo ni mfungaji wa zama zote wa Barcelona akiwa na mabao 523 katika mashindano yote.
  3. Messi aliweka rekodi ya kwanza katika Ligi ya Mabingwa Ulaya kufunga mabao matano katika mechi moja. Rekodi hiyo aliiweka mwaka 2012 dhidi ya Bayer Leverkusen.
  4. Katika El Clasico amekuwa mchezaji anayeongoza kwa kufunga mabao mengi katika historia ya miamba hiyo katika mashindano yote akifunga mabao 24.
  5. Messi amekuwa mchezaji wa kwanza nje ya Hispania aliyecheza mechi nyingi katika klabu ya Barcelona kuliko mchezaji mwingine, akicheza mechi 602.
  6. Msimu wa 2011/12 aliweka rekodi ya kufunga mabao 50 katika La Liga hivyo kuwa mchezaji bora kuwahi kutokea katika ligi hiyo kwa msimu mmoja.
  7. Pia Messi amekuwa mchezaji aliyefunga mfululizo katika historia ya La Lig, akifanya hivyo katika mechi 21 hivyo kuwa rekodi ya kipekee.

Lionel Messi

REKODI ZA MESSI KATIKA HISABATI

602– Mechi alizocheza akiwa na Barcelona

427-Mechi alizoshinda

106– Mechi alizotoka sare

69– Mechi alizopoteza

523-Mabao aliyofunga

423– Mabao aliyofunga kwa mguu wa kushoto

76– Mabao aliyofunga kwa mguu wa kulia

22– Mabao aliyofunga kwa kichwa

2– Mabao aliyofunga kwa maeneo mengine ya mwili.

197– Pasi za mwisho

Akiwa na miaka 17 alianza kuitumikia Barcelona, na kufunga bao la kwanza akiwa na Barcelona pia alitwaa taji la kwanza la La liga akiwa na Barcelona.

Haikutosha akiwa na miaka 18 alianza kuitumikia timu ya taifa ya Argentina na kufunga bao la kwanza, kisha kutwaa taji la pili la La liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na taji la kwanza la Supercopa de Espana. Akiwa na miaka 19 alifunga hat trick yake ya kwanza katika El Clasico wakitoka 3-3 pia alitwaa taji la pili la Supercopa de Espana.

Huyo ni Lionel Messi kwa ufupi.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni