Makala Maalumu

Mfahamu Alphonce Felix Simbu

Tarehe August 7, 2017

Alphonce Felix Simbu akimaliza wa tatu katika mbio za dunia Agosti 6, 2017 jijini London.

Alphonce Felix Simbu akimaliza wa tatu katika mbio za dunia Agosti 6, 2017 jijini London.

Alphonce Felix Simbu alizaliwa Februari 14, 1992 katika kijiji cha Nampando mkoani Singida Mashariki (Ikungi), akiwa ni mtoto wa saba kati ya kumi (10) wa Mzee Felix Simbu.

Alphonce Felix Simbu atwaa medali ya shaba IAAF 2017

Wakati fulani aliwahi kukaririwa akisema medani ya riadha katika kategori yam bio alianza akiwa Shule ya Msingi Nampando kutokana na ushawishi wa Mwalimu Juma Jambau aliyekuwa akifundishwa shule jirani ya Lighwa. Mwaka 2003 akiwa darasa la tano alijaribu kukimbia kilometa tano ambazo zilifanyika Singida kwa udhamini wa Puma baada ya hapo aliacha na kuendelea na mambo mengine.

Mwaka 2005 alishiriki mbio za Babati Half Marathon ambazo zilikuwa na kilometa tano ndani yake kwa ajili ya wanafunzi. Alifanikiwa kushika nafasi ya tano.

“Mbio hizi nakumbuka tena nilikimbia pekupeku (bila viatu), nilifanikiwa kushika nafasi ya tano, mbio hizi zilisaidia kipaji changu kuonekana na kupata ufadhili na kujiunga na shule ya vipaji maalumu ya Winning Spirit ya jijini Arusha.”- Alphonce Felix Simbu

Aidha Simbu aliwahi katika kipindi cha kati ya 2013-2014 kukaa chini ya klabu ya riadha ya Holili Youth (HYAC) iliyopo Kilimanjaro chini ya kocha Timothy Kamili.

Akiwa na HYAC alishiriki mbio mbalimbali akisaidiwa vifaa na ushauri ikiwamo mbio ya Sokoine Min Marathon mwaka 2014 ambayo alishika nafasi ya pili.

Mwanaridha huyo aliwahi kushiriki mbio za kilometa 21 za Dar Rotary mwaka 2013 na zile za Rock City ambazo zote alishinda kwa kushika nafasi ya kwanza.

Simbu alisema mwaka 2011 aliumwa sana, lakini alishiriki kiunyonge michuano ya Afrika (All Africa Games) kwenye kategori ya mbio za mita 10,000 ambako hakufanya vizuri. Mwishoni mwa mwaka 2012 alikwenda Brazil na kushiriki mbio za Brasilia kilometa 10 za barabara ambako alishika nafasi ya kumi (10).

Mwaka 2014 alishiriki mbio ya Gyongoy Half Marathon Korea Kusini na kushika nafasi ya pili kabla ya kwenda kambini Ethiopia akiwa na timu ya taifa ya Tanzania kujiandaa na michezo ya Jumuiya ya Madola ambako alipatwa na majeruhi.

Mwaka 2015 afya yake iliimarika na kuanza kushiriki mazoezi kisha alishiriki mbio za Kilimanjaro Marathon na kushika nafasi ya nne na baadaye Mbio za Nyika za Dunia za Gyuyang nchini China ambako alishika nafasi ya 49 katika kilometa 12. Baada ya hapo alianza maandalizi ya Mbio za Dunia za mwaka 2015 ambapo alikimbia marathoni yake ya kwanza ya Gold Coast Airport Australia na kushika nafasi ya sita akitumia saa 2:12.01 na kufuzu.

Agosti 22, 2015 alishiriki Mbio za Dunia za IAAF jijini Beijing alikoshika nfasi ya 12 akitumia saa 2:16.57

Machi 6 mwaka 2016 alishiriki mbio za Lake Biwa nchini Japan na kupata muda mzuri wa saa 2:09.19 akishika nafasi ya tatu. Muda huo ulimpeleka katika Mashindano ya Olimpiki mwaka 2016 yaliyofanyika Rio de Janeiro nchini Japan na Desemba 2016 alizama katika kambi iliyopo West Kilimanjaro. Katika michuano hiyo ya Rio alishika nafasi ya tano.

Mwaka 2017 ulianza kwa nyota yake kung’ara katika mbio za Mumbai alikotwaa taji hio na Aprili 23 mwaka huu London Marathon alitumia saa 2:09.10

Imetayarishwa na Jabir Johnson

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni