Makala Maalumu

Matumaini ya Argentina, Ghana, Chile, Australia kufuzu Kombe la Dunia yapo?

Tarehe October 9, 2017

Lionel Messi

Mbio za kufuzu Kombe la Dunia 2018 nchini Russia ni kama zimefikia mwisho. Russia imefuzu kama mwenyeji na mataifa mengine 11 tayari yameshafuzu. Lakini kuna mataifa ambayo yanasubiri mechi zao za mwisho katika kimuhemuhe hicho cha kufuzu siku zijazo miongoni mwa hizo ni Argentina, Ghana, Chile na Australia.

AFC – Timu 46

Zilizofuzu: Korea Kusini, Saudi Arabia, Iran, Japan

Katika shirikisho la Soka la Asia mchezo unaosubiriwa ni ule baina ya Syria na Australia. Zilizotoka sare ya 1-1 katika mkondo wa kwanza. Inaangaliwa zaidi Australia ambayo ina wachezaji watano wanaocheza soka la kulipwa nchini England akiwamo Aaron Mooy nyota anayehudumu Huddersfield ambaye ameshiriki mara tatu mfululizo mbio.

CONCACAF – Timu 35

Zilizofuzu: Mexico

Costa Rica ilikuwa mwenyeji wa Honduras wikiendi iliyopita ikitarajia kuwa itafuzu kwenda Russia lakini haikuwa hivyo. Marekani ikiwa na nyota wa Stoke City Geoff Cameroon ili ifuzu itapaswa kuizabua Trinidad & Tobago. Panama ipo nafasi ya nne ikisalia na mchezo dhidi ya Costa Rica ili matumaini ya kufuzu yawe hai.

CAF – Timu 54

Zilizofuzu: Nigeria

Nigeria imefuzu baada ya kuizabua Zambia. Pia Super Eagles inajivunia kuwa na nyota wake wane wanaosakata kabumbu Ligi Kuu ya England ambao ni Ahmed Musa, Alex Iwobi, Kelechi Iheanacho na Victor Moses. Bao pekee la Iwobi liliipa Nigeria kufuzu. Washindi wa makundi mengine matano Tunisia, Ivory Coast na Misri bado wako imara. Lakini kundi D ambalo yupo Senegal linaonekana lipo wazi kwa Cape Verde na Burkina Faso. Algeria na mabingwa wa Afrika Cameroon wameshatolewa huku Ghana ikiendelea kupambana vikali kuhakikisha nafasi yake haipotei.

CONMEBOL – Timu 10

Zilizofuzu: Brazil

Nje ya Neymar anayeiongoza Brazil kwenda Russia huenda ndio  kundi pekee ambalo linaweza kuwa na habari za kusikitisha huku ikisalia mzunguko mmoja. Uruguay ana pointi 28 atakuwa nyumbani kucheza na Bolivia, Chile ina pointi 26 huku akitarajia kupambana na Brazil ugenini, Colombia ina pointi 26 itakapocheza na Peru ugenini na Peru yenyewe ikiwa na alama 25. Sasa ngoma ipo kwa Argentina yenye nyota Lionel Messi itakapokuwa nyumbani kuikabili Ecuador huku Paraguay ikiwa na pointi 24 itakapowakaribisha Venezuela kesho Jumanne. Hivyo timu tano zinapambana. Katika uhalisi Messi anaweza kulikosa Kombe la Dunia mwaka ujao.

OFC – Timu 11

New Zealand ilijipatia mteremko kwa uwiano wa mabao 8-3 dhidi ya Solomon Islands huku nyota wa Burnley Chris Wood akitupia hat trick katika mzunguko wa kwanza.

Hata hivyo Oceania hao watakuwa wakisubiri kuona Messi na wenzake watakavyokuwa wakipanda  mlima wa Ecuador hapo kesho.

Imetayarishwa na Jabir Johnson.

Neymar dos Santos katika mchezo wa kuwani kufuzu Kombe la Dunia 2018 dhidi ya Paraguay.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni