Michezo/Sports

Lwandamina atimka,Viongozi Yanga washikwa na butwaa

Tarehe April 11, 2018

Kocha wa Yanga George Lwandamina.

Kocha wa Yanga George Lwandamina anadaiwa kuondoka nchini Tanzania ambapo tetesi zinasema anarejea Zesco United ya kwao na atatambulishwa Alhamisi.

Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amsema  kwamba Lwandamina hajatokea mazoezini leo asubuhi bila sababu na wanamtafuta hapatikani.

“Mimi sijui kaenda wapi, kwa sababu hajaniaga. Hizo hizo habari (za kwenda Zambia) wewe ndiyo unaniambia,”amesema Mkwasa baada ya kuulizwa na Bin Zubeiry Sports – Online juu ya kocha huyo kurejea kwao, Zambia.

Inadaiwa kwamba Zesco United imeamua kumrejesha kocha wake huyo baada ya mafanikio yake Tanzania ndani ya miaka miwili, akiiwezesha kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu uliopita na sasa inakaeribia kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni