Michezo/Sports

Liverpool kuvunja rekodi ya mwaka 2002 kesho?

Tarehe September 25, 2017

INFOGRAPHIC: Kundi E Septemba 26, 2017

KUNDI E

Sevilla? – ? Maribor

Spartak Moscow? – ? Liverpool

Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp atakuwa na kazi nyingine ya ziada baada ya kupata ushindi dhidi ya Leicester City mwishoni mwa juma lililopita katika dimba la King Power wa mabao 3-2. Kwa mara ya mwisho Liverpool kushinda nyumbani na ugenini dhidi ya Spartak ilikuwa mwaka 2002.

Mwitaliano Massimo Carrera na vijana wake hawatakuwa na muda wa kufurahia jua isipokuwa ni kuondokana na ombwe la kuanza vibaya msimu huu ambao wameshinda mechi tatu katika michezo 11, wakitupwa alama 13 nyuma ya Zenit St. Petersburg wanaoongoza ligi kuu nchini Russia.

Hata hivyo uwepo wa Mbrazil Philippe Coutinho utaendelea kutoa matumaini makubwa kwa kikosi cha Klopp. Hilo lilijirihirisha kaika mchezo dhidi ya Leicester City pale alipotoa krosi iliyomfikia Mohamed Salah ambaye alizifumania nyavu na kuwapa Majogoo hao wa Anfield uongozi dhidi ya Mbweha.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni