Michezo/Sports

Kumekucha Dar Rotary Marathon

Tarehe October 12, 2017

Wanariadha wa mbio za kilometa 10 katika Dar Marathon mwaka 2016.

Mashindano ya Mbio Dar Rotary Marathon yanatarajiwa kufanyika wikiendi hii jijini Dar es Salaam kwa kuwaleta wanariadha mahiri katika kilometa 21 na 42.

Mbio hizo zinafanyika kwa mara ya tisa mfululizo tangu kuanzishwa kwake mwaka 2009.

Matembezi hayo hufanyika kila mwaka kuadhimisha kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Nyerere katika viwanja vya Greens, Oystebay jijini humo.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari hapo jana jijini, Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya Rotary Dar Marathon Bi. Catherinerose Barretto alisema “Kuna mambo mapya yameongezeka katika ushiriki wa matembezi mwaka huu, kwa mara ya kwanza tutakuwa na marathon iliyokamilika ya km 42.2, pia tutaongeza urefu wa mzunguko kwa waendesha baiskeli kutoka km 21.1 kufikia km 42.2. Matembezi ya km 9 mwaka huu yatarefushwa kufikia km 10, matembezi ya km 5 tu ndio yatabaki kama yalivyo

Mbio na matembezi ya rotary Dar Marathon pamoja na kuwa na lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya shughuli mabalimabali za kijamii, pia yamekuwa yakiboreshwa kila mwaka na kuvutia washiriki wengi wakiwemo wa kimataifa.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni