Michezo/Sports

Kingue kuikosa Mwadui wikiendi hii

Tarehe October 12, 2017

Kiungo Mkabaji wa Azam FC Stephan Kingue

Kiungo Mkabaji wa Azam FC Stephan Kingue ataukosa mchezo wake dhidi ya Mwadui FC utakaochezwa mkoani Shinyanga wikiendi hii.

Azam FC imeshawasili katika ardhi ya Shinyanga kuwakabili wenyeji wao, huku Kocha Aristica Cioaba akiwa na matumaini tele ya kuibuka na ushindi katika mtanange huo licha ya kumkosa Kingue.

“Wachezaji wote wapo tayari hakuna mchezaji majeruhi na morali ipo juu, wote tunaamini kama tutafanya kazi kama familia huku tukiweka tahadhali kwa wapinzani wetu, huwa nawaambia kuwa timu zote zinacheza mpira mzuri haijalishi ni Yanga ama timu yoyote, cha msingi ni kumuheshimu mpinzani na mchezo wenyewe, ninachohitaji ni ushindi siku ya Jumamosi na kupata pointi tatu,” alisema.

Azam FC ilisema Kingue bado hajapona vizuri majeraha ya mgongo.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni