Michezo/Sports

Jerrry Muro atoa neno ushindi wa Simba

Tarehe January 11, 2017

Jerry Muro na Haji Manara

Jerry Muro na Haji Manara

 

 

Msemaji wa timu ya Yanga, Jerry Muro aliyepo kifungoni ameshindwa kujizuia na kulazimika kutoa neno kufuatia ushindi walioupata watani wao Simba hapo jana kwa kuwachabanga goli 4-2 njia ya matuta baada ya kutofungana ndani ya dakika 90.

Ushindi wa Simba ulipata visiwani Zanzibar ambapo michuano ya Mapinduzi Cup inaendelea na sasa kwa ushindi huo wanatarajia kucheza na Azam katika mchezo wa fainali hapo Januari 13.

Muro ametumia mtandao wa kijamii kuwaambia Simba kuwa ni afadhali wameshinda mechi hiyo kwani endapo wangefungwa wangekasirika na kuvunja Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ikiwa ni utani wa pale Simba walipofanya vurugu na kuvunja viti katika uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam.

15894381_1326369554073126_4894137977595002151_n

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni