Michezo/Sports

JB ‘awazodoa’ vibaya Yanga

Tarehe January 11, 2017

JB (kushoto) akiwa amekaa chini akiendelea kutazama mpambano kati ya Simba na Yanga, na kushuhudia timu yake Simba ikiwabamiza watani wake Yanga goli 4-2 kwa matuta.

JB (kushoto) akiwa amekaa chini akiendelea kutazama mpambano kati ya Simba na Yanga, na kushuhudia timu yake Simba ikiwabamiza watani wake Yanga goli 4-2 kwa matuta.

Msanii maarufu wa Bongo Movies Jacob Steven ‘JB’ amesema kitendo cha timu ya Yanga kubamizwa na watani wao Simba sasa imekuwa jambo la kawaida sana na kudai kuwa wana jangwani hao wataendelea kupokea kichapo kila mara watakapokuwa wanakutana na Simba.

“Si ajabu, Yanga kufungwa na Simba ni kitu cha kawaida na wataendelea kufungwa tu. Tukitoka kwenye mashindano haya tunarudi Dar ambako tutakutana tena kwenye ligi huko pia wasubiri kichapo kingine,” amekaririwa akisema JB.

JB ambaye ni shabiki wa kutupwa wa Simba alikuwepo uwanja wa Amaan mjini Unguja kuishuhudia timu yake wakati ikipambana na Yanga kwenye mchezo wa nusu fainali ya kombe la Mapinduzi.

Mechi hiyo ilimalizika kwa Yanga kuchezea goli 4-2 kwa mikwaju ya penati baada ya kutoshana nguvu ya bila kufungana hadi dakika 90 za mchezo huo zinamalizika.

Simba itacheza na Azam FC mchezo wa fainali kutafuta bingwa mpya wa michuano ya 11 ya Mapinzuzi kwa mwaka 2017 hapo Januari 13.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni