Michezo/Sports

Italia yashindwa kufuzu Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1958

Tarehe November 14, 2017

Wachezaji wa kikosi cha timu ya taifa ya Italia wakiwa katika masikitiko baada ya kushindwa kufuzu fainali za Kombe la Dunia.

Timu ya Taifa ya Italia imeshindwa kufuzu Kombe la Dunia 2018 kwa mara ya kwanza tangu ilipofanya hivyo mwaka 1958 baada ya kutolewa kwa uwiano wa bao 1-0 hivyo kuwaacha wapenzi na mashabiki wa Azzuri wakitokwa na machozi baada ya mchezo huo.

FT: ITALIA 0-0 (0-1) SWEDEN

Kushindwa kufuzu kwa Italia kunamfanya mlinda mlango Gianluigi Buffon kumaliza medani ya soka akiwa amecheza mechi 175 akiwa na kikosi hicho. Ikumbukwe Buffon alitangaza kuwa atastaafu kuitumikia timu ya taifa baada ya Kombe la Dunia.

Kikosi cha Kocha Gian Piero Ventura kimeshindwa kuwatoa Sweden katika mchezo huo hivyo kumfanya Buffon kukosa fainali za sita za Kombe la Dunia katika maisha yake.

Mlinda mlango Gianluiggi Buffon akiwapungia mkono mashabiki kwa masikitiko baada ya kushindwa kufuzu.

Buffon akiagana na mlinda mlango wa AC Milan Gianluiggi Donnarumma baada ya mchezo huo.

Wachezaji wa Sweeden wakiwa katika furaha baada ya kufuzu.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni