Makala Maalumu

Inahitajika akili kumdhibiti Ajibu Oktoba 28

Tarehe October 25, 2017

Ibrahim Ajibu ndio habari ya mjini kuelekea mechi ya watani wa jadi Oktoba 28 mwaka huu katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Kama ilivyokuwa katika Ngao ya Jamii Agosti mwaka huu wakati wa ufunguzi wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2017/18. Ajibu ndiye mchezaji ambaye Simba SC inamwogopa kwa sasa kutokana na kuwa msimu uliopita alikuwa akiitumikia Simba kwa mafanikio makubwa hata kuchukua taji la Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania Bara (ASFC). Hiyo ndiyo sababu hata katika mechi ya ngao ya Jamii alibanwa vya kutosha.

AJIBU ALIBANWA HIVI

Mlinzi wa kati Salim Mbonde alikuwa ngao muhimu ya kumpoteza Ajibu. Ulinzi huo ulikamilika pale Method Mwanjali, Ali Shomari na Mzamiru walipoongezeka na kuziba mianya na njia zote za Ajibu kufanya vile atakavyo. Ulinzi huo ulimpa mlinzi wa kushoto Erasto Nyoni kupata mwanya wa kupanda mbele kushambulia hali iliyowarudisha nyuma Ajibu kwa ajili ya kuzuia hivyo kuchelewa kupanda mbele kwa ajili ya kushambulia.

ITAWEZEKANA OKTOBA 28?

Mbonde alipata majeruhi katika mechi dhidi ya Mtibwa hivyo Yusuf Mlipili na Juuko Murshid walibadili nafasi yake. Ambapo walifanya kazi nzuri katika mchezo dhidi ya Njombe Mji walipotoka kifua mbele kwa mabao 4-0. Mzamiru alipata nafasi ya kupanda mbele huku dimba la chini akimwacha Jonas Mkude. James Kotei hakucheza mchezo huoinawezekana yalikuwa malengo ya Kocha Joseph Omog kumpumzisha raia huyo wa Ghana kwa ajili ya kumdhibiti Ajibu.

Ajibu akitafuta namna ya kuwatoka walinzi wa Simba SC Method Mwanjali na kiungo wake Mzamiru Yassin katika mchezo wa Ngao ya Jamii Agosti 2017

NAFASI YA EMMANUEL OKWI

Mshambuliaji wa Simba SC Emmanuel Okwi anaongoza kwa ufungaji kwa sasa katika Ligi Kuu Tanzania Bara akiwa amepachika wavuni mabao saba (7). Mabao hayo ameyafungia yote katika Uwanja wa Uhuru hivyo anaweza akaendeleza kasi ya kufumania nyavu katika dimba hilo. Hata wachezaji wa Young Africans wanajua kuwa wakifanya makosa mbele ya Okwi itawagharimu. Kila timu imejiweka katika tahadhari kubwa.

Imetayarishwa na Jabir Johnson.

Mashabiki Young Africans wakiwa na bango la Ibrahimu Ajibu.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni