Makala Maalumu

Hamad Ndikumana ni nani?

Tarehe November 16, 2017

Hamad Ndikumana enzi za uhai wake.

Kumekuwa na mkanganyiko kuhusu Ndikumana miongoni mwa wafuatiliaji wa masuala mbalimbali ya michezo Tanzania na Afrika kwa ujumla. Hiyo inatokana na kifo cha mwanasoka wa zamani wa Rwanda aliyewahi kufanya kazi nchini Tanzania.

Huyo sio mwingine ni Hamad Ndikumana. Mwanasoka huyo ni yule aliyekuwa mume wa muigizaji maarufu nchini Irene Uwoya. Ndikumana aliwahi kuitumikia klabu ya Stand United ya Shinyanga ambayo ipo katika Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2017/18.

Nyota huyo amefariki dunia akiwa na miaka 39 kutokana na kile kinachodaiwa kuwa maradhi ya moyo yaliyojificha. Uhusiano wake na Uwoya ulikuwa maarufu mno nchini kutokana na kukutana na misukosuko ya kila mara. Muda mfupi baada ya taarifa za kifo chake, idadi kubwa ya watu katika mitandao ya kijamii walieleza kushitushwa na tukio kila mmoja akieleza la kwake.

Hamad Ndikumana is no more.

Daktari ya klabu ya Rayon Sports, Charles Mugemana alikaririwa akisema Ndikumana hakuwa kulalamika kuhusu tatizo la afya na siku moja kabla ya kifo chake alifanya mazoezi na timu hiyo. Taarifa nyingine zilidaiwa kuwa katika eneo alilokuwa akiisha la Nyakabanda, Nyarugenge alimwambia jirani yake yake kuwa ana maumivu makali ya kifua kabla ya kuaga dunia. Ndikumana alikuwa miongoni mwa walinzi bora kuwahi kutokea Rwanda kabla ya kustaafu mwaka 2015.

Alianza kufundisha timu ya mtaani ya Espoir FC. Msimu uliopita alikuwa kocha msaidizi wa Musanze FC akimsaidia Kocha Mkuu Sosethen Habimana ambaye ni mlinzi wa zamani wa Rayon Sports. Hadi mauti yanamkuta alikuwa Kocha msaidizi wa Rayon Sports akisaidiana majukumu na kocha mkuu Olivier Karekezi.

Ndikumana alizikwa Novemba 15, 2017 katika makaburi ya Nyamirambo. Kifo chake kimekuja ikiwa siku moja baada ya mchezaji mwingine wa zamani wa Amavubi Bonaventure ‘Gangi’ Hategekimana kulazwa Hospitali ya Kabutare kutokana na maradhi ya muda mrefu. Ndikumana alianza kutambana katika medani ya kandanda baada ya kujiunga na Rayon Sports msimu wa 1998/99.

Aliitumikia timu ya taifa ya Rwanda mitanange 51 huku akiweka rekodi ya kucheza fainali za Mataifa ya Afrika nchinio Tunisia mwaka 2004.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni