Michezo/Sports

FIFA yaongeza idadi ya timu kombe la dunia hadi 48

Tarehe January 10, 2017

131021122824-world-cup-trophy-horizontal-large-gallery

Shirikisho la Mpira Miguu wa Miguu Duniani (FIFA) limetangaza rasmi kuwa kuanzia Kombe la Dunia la kuanzia mwaka 2026 litakuwa linashirikisha timu 48 zitakazounda makundi 16 yenye timu tatu kila kundi kufuatia kura zilizopigwa Mjini Zurich, Uswisi.

Idadi hiyo itajumuisha timu tisa kutoka bara la Afrika.

Uamuzi huu uliibua mjadala mzito kwa siku za hivi karibuni huku baadhi ya nchi zikitaka idadi ya timu shiriki iendelee kubakia ileile ya mwanzo ya timu 32.

Nafasi za timu za Ulaya kufuzu Fainali za Kombe la Dunia zitaongezeka kutoka 13 hadi 16, wakati Afrika na Asia zitaingiza timu tisa tisa kila Bara kutoka tano kwa Afrika na nne za Asia.

Kutakuwa na jumla ya mechi 80 katika mfumo mpya kutoka mechi 64 katika mfumo wa sasa wa timu 32.

Ongezeko la timu linamaanisha pia kutakuwa ongezeko la mapato kwa FIFA kutoka Pauni Milioni 521 hadi Bilioni 5.29 katika mfumo wa timu 48.

c1zqw8sxuaallby

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni