Michezo/Sports

Chiellini, De Rossi, Barzagli kufuata nyayo za Buffon?

Tarehe November 14, 2017

Buffon akimfariji Leandro Bonucci baada ya mchezo dhidi ya Sweden.

Baada ya kushindwa kufuzu kucheza Kombe la Dunia Giorgio Chiellini, Andrea Barzagli na Daniele de Rossi wanaweza kuthibitisha nao kustaafu kuitumikia timu ya taifa hivyo kufuata nyayo za mkongwe mwenzao Gianluiggi Buffon.

Kinachoonekana baada ya kushindwa kufuzu kwa mabingwa hao mara nne wa Kombe la Dunia ni kwamba Chiellini, De Rossi na Barzagli wanaweza kutangaza kuachana na majukumu ya kitaifa.

Buffon ameshinda michezo 175 akiwa na Italia pia akitwaa Kombe la Dunia mwaka 2006 baada ya ushindi wa changamoto ya mikwaju ya penalti mjini Berlin dhidi ya Ufaransa. Pia Buffon akiwa mlinda mlango namba moja wa Juventus alikuwamo katika kikosi kilichoshindwa kutwaa taji la Ulaya mwaka 2000.

Aidha Buffon alikuwa katika kichapo cha mabao 4-0 dhidi ya Hispania kwenye Euro 2012.

Gianluiggi Buffon

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni