Michezo/Sports

Beki wa Arsenal agundulika kuwa na HIV

Tarehe October 4, 2017

Mlinzi wa zamani wa Klabu ya Arsenal, Raia wa Ivory Coast, Emmanuel Eboue amekwama katika uhamisho wake kwenda klabu moja huko Uturuki na dili hilo kuwekwa kiporo baada ya vipimo vyake vya afya kuonesha mambo tofauti katika damu yake.

Kwa mujibu wa Chris Wheatley kutoka mtandao wa Goal, Wakala wa Eboue, Tekin Birinci ambaye alikuwa kama mtu wa kati katika dili hilo amethibitisha kuwa Eboue kwa sasa anachunguzwa nchini Uingereza na kukanusha vikali habari ya vyombo vya habari vya Uturuki ya kuwa mchezaji huyo mwenye miaka 34 amekutwa na virusi vya ukimwi (HIV).

“Eboue alisaini kwa klabu hiyo ya Uturuki , na kama ulivyo utaratibu, ilibidi kumchukua vipimo vya afya. Walikuta mambo yasiyo kawaida katika damu yake na hivyo hawakutoa leseni na tukafanya uamuzi wa kumpeleka Uingereza kufanya vipimo pale,”amesema.

Ameongeza kuwa kwa sasa sio vyema kusema kuwa mchezaji huyo ana HIV, na kwamba vyombo vya habari vya Uturuki vinakosea.

“Nilielezea vizuri suala la Eboue siku mbili zilizopita, lakini hata kama jambo hilo ni kweli, halipaswi kutangazwa kwa namna hiyo ambayo vyombo vya habari vya Uturuki vimefanya,” ameongeza.

Raia huyo wa Ivory Coast amecheza mechi 215 akiwa katika uzi wa Arsenal katika kipindi cha misimu sita alichokuwa na washika bunduki hao wa London na kufanikiwa kufunga magoli 10 na kutoa pasi za mwisho ‘assists’ 20.

Mwaka 2001, mkali huyo aligeukia kwa mabingwa wa Uturuki, Galatasaray, na kufanikiwa kushinda makombe mawili ya ligi kuu ya Uturuki katika kipindi cha miaka minne alichoichezea klabu hiyo.

Endelea kuwa nasi kwa taarifa zaidi juu ya hili.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni