Michezo/Sports

Azam wamchukua Mromania kuwa kocha mkuu

Tarehe January 10, 2017

c1z9cbjxgaadkbc

Klabu ya Azam FC, inadaiwa kuingia mkataba na Raia wa Romania, Aristica Cioaba kuwa kocha mkuu wa klabu hiyo kwa muda wa miezi sita ili kuangalia ufanisi wake.

Kwa sasa Mromania huyo yupo visiwani Zanzibar akiitazama klabu hiyo ikiendelea na michuano ya kombe la Mapinduzi.

Afisa habari wa Azam FC Jafar Idd amesema Aristica Cioaba atasaidiwa na makocha wazalendo ambao wanaiongoza Azam kwa sasa wakiongozwa na Idd Cheche.

Hivi karibuni, Azam FC iliamua kuwafukuza makocha wake wa kigeni wakiongozwa na kocha mkuu Zeben Hernandez kutoka Hispania.

Uongozi wa Azam FC uliwatimua makocha hao baada ya pande zote mbili kukubaliana kuvunja mkataba kutokana na matokeo mabaya kwenye ligi tangu walipowasili hasa mfululizo wa matokeo mabovu kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu tangu ‘wahispania’ hao walipokabidhiwa mikoba ya kuinoa timu hiyo baada ya Stewart Hall kubwaga manyanga.

 

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni