Michezo/Sports

Droo ya CHAN 2018 leo jijini Rabat, Morocco

Tarehe November 16, 2017

Kamati ya Maandalizi ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN 2018) imepanga droo na ratiba ya mashindano ifanyike Sofitel mjini Rabat baada ya kukamilika kwa timu 16 za kushiriki mashindano hayo, kufuatia Rwanda kufuzu ikiitoa Ethiopia katika mechi ya mwishi ya mchujo.

Timu zilizofuzu ni pamoja na wenyeji, Morocco, Angola, Ivory Coast, Libya, Cameroon, Guinea, Nigeria, Zambia, Kongo, Uganda, Rwanda, Sudan, Burkina Faso, Equatorial Guinea, Mauritania na Namibia.

Kamati pia imethibitisha michuano itaanza Januari 13 hadi Februari 4 mwaka 2018 katika miji ya Casablanca (Kundi A), Marrakech (Kundi B), Tangier (Kundi C) na Agadir (Kundi D).

Mechi ya ufunguzi na fainali zitafanyika kwenye Uwanja wa Mohamed V Complex mjini Casablanca, ambao pia ulitumika kwenye mchezo wa marudiano wa fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika 2017.

Kenya ilinyang’anywa uenyeji na Morocco kuchukua nafasi hiyo.

Droo hiyo itakuwa kama ifuatavyo;

Pot 1: Morocco (wenyeji), Angola, Cote d’Ivoire, Libya

Pot 2: Cameroon, Guinea, Nigeria, Zambia

Pot 3: Congo, Uganda, Rwanda, Sudan

Pot 4: Burkina Faso, Equatorial Guinea, Mauritania, Namibia

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni