Makala Maalumu

Wasanii wavunja ukimya kuhusu Hali ngumu ya Maisha

Tarehe October 22, 2017

Shamsa ford

Wasanii wavunja ukimya kuhusu Hali ngumu ya Maisha

Hatimaye baada ya kilio cha kuwepo hali ngumu ya maisha chini utawala wa awamu ya Tano,Wasanii mbalimbali wameanza kuonesha hisia zao na kuitaka Serikali kuangalia namna ya kuboresha maisha ya wananchi.

Mmoja wa wasanii aliyevunja ukimya ni Muigizaji wa filamu bongo Shamsa Ford ambaye amemtaka Rais Magufuli alegeze kidogo kamba ili hali ya maisha ikae sawa kiuchumi

Kwenye ukurasa wake wa instagram Shamsa ameandika ujumbe akisema hali siku hizi imekuwa ngumu kiasi cha watu kushindwa kufanya yale waliyoyazoea kwenye maisha yao ya kila siku, hata biashara imekuwa ngumu zaidi, na kama kunyooka ilipofikia imetosha.

Mr President tunaomba ulegeze kidogo hali mbaya baba, tumeshashika adabu sasa hivi na tunaheshimu pesa .Buku sasa hivi tunaiita elfu moja, yaani sijapata hata mialiko ya birthday kubwa kubwa kama ambavyo wanafanyaga. Mbwembwe hakuna tunaishia kupostiana instagram tu. Baba naomba usikie kilio changu hali mbaya sitaki kurudi iringa kulima mjini patamu jamani. Biashara imekuwa ngumu sana wateja hakuna jamani …Baba Tuonee huruma jamani tumepauka kweli yaani mpaka ukimuona mwenzio unakimbia”, ameandika SHamsa Ford.

Licha ya Shamsa Ford kumuangukia Rais Magufuli,wasanii wengine waliowahi kuvunja ukimya kuhusu hali ngumu ya maisha ni Msanii Matonya aliyeachia wimbo unaoitwa ‘Mr Legeza’ ambapo katika wimbo huo amelezea hali halisi ya maisha ilivyo chini ya utawala wa awamu tano na kumtaka Rais Magufuli kuangalia namna ya kuyafanya maisha yawe rahisi kwa watu wa kawaida.

Mwanamuziki Mwingine ni Roma Mkatoliki kupitia wimbo wake wa Zimbabwe amesema hali ya maisha ya wananchi sio rahisi kama awamu za uwatala wa marais wengine zilizopita.

Wakati Wananchi,Wanasiasa,wasanii na Wafanyabiashara wakilia hali ngumu, Rais Magufuli amewataka  wananchi kuvumilia kwa kuwa nchi inapita katika Mageuzi.

Aidha, Rais Magufuli katika utawala wake wa awamu ya tano amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuboresha huduma katika shirika la ndege la umma ATCL kununua ndege mpya, kupambana na watumishi hewa, kuondoa vyeti na kupambana na rushwa.

Katika sekta ya Madini Rais Magufuli amefanikiwa kuanika uozo katika biashara ya madini, na sasa mchakato umefikia Serikali kuwagawana asilimia 50 kwa 50 na wawekezaji kwenye madini.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni