Makala Maalumu

Ukeketaji ni Tishio Tarime,Wasichana 800 wakeketwa kwa Mwezi

Tarehe January 7, 2017

ukeke

Wasichana zaidi ya 800 walikeketwa kaskazini mwa Tanzania mwezi uliopita, mkuu wa wilaya ya Tarime Glorious Luoga amesema.

Je Ukeketaji ni nini?

Ukeketaji ni kitendo cha  ukataji sehemu za siri za wasichana na wanawake na hufanywa na baadhi ya Makabila hapa nchini wakiwemo  wakurya, Wagogo, Wajita, Wamasai pamoja na Wanyaturu.

Kwa mujibu wa Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) inakadiriwa  kuwa wanawake milioni 91 na nusu wamekeketwa. Kati ya hao Milioni 12 na robo wana umri mdogo wa miaka 10 hadi 14.

Nazo Takwimu za Demographia  Mwaka 2012 zinaonesha kuwa ukeketaji upo kwa kiasi kikubwa katika mikoa kama ifuatavyo:

ukeketaji

 

Aidha, Ukeketaji  hufanyika ingawa polisi wamekuwa wakikabiliana na utamaduni huo. Eneo la Tarime, wasichana hukeketwa wakiwa na umri wa kati ya miaka 12 na 17.

Aidha, hivi karibuni  Wanawake 12 wanaotuhumiwa kuhusika katika kuwakeketa wasichana hao wamekamatwa na maafisa wa polisi.

Inakadiriwa kwamba nchini Tanzania, wasichana na wanawake 7.9 milioni wamekeketwa.

Novemba, kabla ya kuanza kwa msimu wa ukeketaji Tarime, Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Tarime, Thomas Mapuli alikuwa ametangaza kwamba polisi wamejiandaa kuwakamata mangariba wote ambao wangejaribu kukeketa watoto wa kike.

“Tumejipanga vizuri na hatutakuwa na huruma kwa atakayekutwa anatenda kosa la ukeketaji,” alisema Bw Mapuli.

Wasichana takriban 140 milioni wamekeketwa maeneo ya Afrika, Mashariki ya Kati na Bara Asia.

Jamii zinazotekeleza utamaduni huu huutazama kama njia ya kuwatakasa wasichana na kuwaandaa kwa maisha ya ndoa.

Lakini utamaduni huo husababisha matatizo mengi ya kiafya. Wengi hufariki wakikeketwa na baadaye wengi hukabiliwa na matatizo sana wanapojifungua.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni