Makala Maalumu

Serikali yatangaza ajira mpya 52, 436,Kada nane zapewa kipaumbele

Tarehe April 13, 2018

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapteni (Mstaafu) Mhe. George H. Mkuchika.

Serikali inatarajia  kuajiri watumishi 52,436 wanaohitajika katika kada mbalimbali nchini kwa ajili kutoa huduma kwa wananchi.

Kwa mujibu wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika alipowasilisha hotuba yake kuhusu makadirio ya bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka ujao wa fedha amesema kada ya afya ina upungufu wa watumishi 14,102, elimu 16,516, kilimo 1,487, mifugo 1,171 na uvuvi 320.

Amesema  Polisi kuna upungufu wa watumishi 2,566, magereza 750, uhamiaji 1,500, zimamoto 1,177, hospitali za mashirika ya kidini na hiari 174 na wengineo 12,673.

Mkuchika ameongeza kuwa katika mwaka huu wa fedha, usimamizi wa ajira za watumishi wa umma umefanyika kwa waajiri wote ambapo watumishi wapya 15,000 wameajiriwa.

Jumla ya walimu 4,348 wa masomo ya sayansi na watumishi 3,152 wa kada ya afya wameajiriwa  ili kuziba pengo lililosababishwa na kuondolewa kwenye Orodha ya Malipo ya Mishahara kwa watumishi wa umma waliobainika kughushi vyeti.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni