Makala Maalumu

Njombe, Iringa na Mbeya vinara maambukizi HIV

Tarehe December 29, 2016

1

Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi nchini Tanzania (TACAIDS) Dkt. Leonard Maboko amesema maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi nchini yameshuka kwa asilimia 20 ambapo watu 54,000 wameambukizwa virusi hivyo kwa mwaka 2015 pekee.

Amesema Ukimwi bado ni janga kubwa duniani na taifa kwa ujumla huku akitaja kundi la wanawake kuwa ndilo lina kiwango cha juu cha maambukizi ya VVU huku mikoa ya Njombe, Iringa na Mbeya ukiwa na kiwango cha juu cha maambukizi hayo kitaifa.

Aidha, alisema serikali imejiwekea mikakati kuhakikisha kuwa waliogundulika kuwa wameathirika wanaanzishiwa dawa, kuhimiza matumizi ya mpira wa kiume, kupunguza maambukizi mapya kwa asilimia 29 na kutoa elimu kwa wanawake wanaojihusisha na ngono, kupunguza maambukizi ya virusi vya Ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni