Makala Maalumu

Mapinduzi Z’bar yalivyokomesha miaka 200 utawala wa Waarabu

Tarehe January 12, 2017

Rais wa kwanza wa Zanzibar, Abeid Amani Karume.

Rais wa kwanza wa Zanzibar, Abeid Amani Karume.

Leo Januari 12,2017 Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Watanzania kwa ujumla  wanaadhimisha  Sikukuu  ya matukio  ya kihistoria ya Mapinduzi Zanzibar.

Mapinduzi ya Zanzibar yalitokea mwaka 1964 ili kumuondoa Madarakani Sultani wa Zanzibar na serikali yake iliyoundwa hususani Waarabu na hatimaye kuweka uongozi Mikononi mwa Waafrika ambao ndio wengi visiwani humo wakikadiriwa kuwa 230,000 kwenye Bahari ya Hindi karibu na Pwani ya Tanganyika.

Kwa mujibu wa Wikipedia Usultani wa Zanziabar ulikuwa umepewa na  Uingereza  Uhuru wake mwaka 1963. Kabla ya hapo Waarabu walikuwa wamefaulu kudumisha katika Mfululizo wa Chaguzi utawala waliokuwa nao tangu zamani za Zanzibar kuwa chini ya Usultani wa Omani.

Chama cha Afro-Shirazi Party(ASP) kilichowakilisha hasa Waafrika kilipo ona kwamba Bungeni kina viti vichache ingawa kilipata 54% za kura katika uchaguzi wa Julai 1963 kilipatana na Chama cha Mrengo wa Kushoto Umma Party.

Ilipofika januari 12,1964 asubuhi na Mapema Mwanachama wa ASP John Okello(1937-1917) kutoka Uganda aliongoza Wanamapinduzi 600-800 wa Kisiwa Kikuu cha Unguja kushinda Polisi wa Nchi kuteka silaha zao.

Pia walielekea Zanzibar Mjini walipo mpindua Sultani Jamshid Bin Abdullah na serikali yake.Waliofariki dunia katika mapigano wanasadikiwa kuwa walifikia 80.

Yalifuata kwa siku kadhaa maangamizi ya Kimbari dhidi ya Waarabu na Waasi wa Asia Kusini.Hadi sasa hakuna hakika kuhusu idadi ya waliouawa ambapo inakadiriwa kuanzia watu 20,000.

Naye Kiongozi wa ASP Abeid Karume asiyekuwa na Msimamo Mkali akwa Rais wa Kwanza wa nchi na wanachama wa Umma Party walipewa nafasi serikali kutokana na mchango wako mkubwa.

Kufikia Machi Okello alikuwa ameshawekwa pembeni na kufikia Aprili kikosi chake kilikuwa  kimeshanyang’anywa silaha.

Mwelekeo wa Kikomunisti wa baadhi katika serikali mpya uliogopesha nchi za Magharibi. Kwa kuwa Zanzibar ilikuwa chini ya athari ya Uingereza, serikali yake iliandaa mipango kadhaa.

Hata hivyo, hofu ya kuundwa serikali ya Kikomunisti haikutimia kamwe, na kwa kuwa wananchi wa Uingereza na Marekani waliweza kuhama bila shida, mipango hiyo haikutekelezwa.

Wakati huo nchi za Kikomunisti za  China,Ujerumani Mashariki na Umoja wa Kisovieti zilianzisha mahusiano ya kirafiki na serikali mpya ya Zanzibar kwa kuitambua rasmi na kwa kutuma washauri.

Karume alifanikisha majadiliano ya kuunganisha Zanzibar na Tanganyika ili kuunda hatimaye muungano wa Tanzania; vyombo vya habari vilitafsiri muungano huo kuwa juhudi za kuzuia Ukomunisti kugeuza Zanzibar.

Mapinduzi yalikomesha miaka 200 ya utawala wa Waarabu Zanzibar, na yanaadhimishwa kila mwaka kama sikukuu ya taifa zima la Tanzania.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni