Makala Maalumu

Mambo 5 yatakayokufanya ufanikiwe mwaka 2017

Tarehe January 1, 2017

best-happy-new-year-pictures

Ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuweza kutufanya sote tuione siku ya leo ambayo ni terehe moja Mwaka mpya wa 2017.

Leo  napenda nizungumzie  mambo ambayo ukiyazingatia  mwaka wa 2017 utakuwa na neema na mafanikio makubwa kwako.

Katika makala hii nimeanisha mambo 5 muhimu ambayo ukiyazingatia yatakusaidia kuweza kuwa na mafanikio kwa mwaka mpya unao anza leo.

Siri kubwa ya kufikia mafanikio unayoyahitaji katika maisha yako ni kuhakikisha unaishi maisha yanayoendana na malengo yako kamwe usiishi maisha ya kuigiza.

Jukumu kubwa unalotakiwa kulitambua ni kuelewa misingi na malengo yako unayotakiwa kuyafuata kila siku bila kupotea.

Haya ni mambo 5 yatakaweza kusaidia kuwa na malengo ambayo yatainua maisha yako.

  1. Jikubali wewe Mwenyewe

Watu wengi wanashindwa kufanikiwa kwa kuwa hawajikubali, wanajishusha thamani kuwa hawawezi. Jipe thamani wewe Mwenyewe katika kila jambo unalolifanya.

  1. Kuwa makini na muda wako

Muda ulionao ni wa thamani sana na kwa bahati mbaya ukishaupoteza umepotea kabisa hauwezi kurudi tena. Hiyo yote ni dalili tosha inayoonyesha kuwa kuna uthamani mkubwa ulio ndani ya muda wako ambao hutakiwi kuupoteza.

Sasa kama wewe unaishi maisha ya kupoteza muda sana, inabidi uelewe kuwa hivyo ndivyo unavyopoteza maisha yako na mwisho wa siku unajikuta ukiishi maisha yasiyo na malengo.

  1. Jifunze kusahau yaliyopita

Kamwe usiwe mtu wa kuendelea kungang’ania mambo mengi ambayo yameshapita ambayo ni sawa na kupoteza muda. Maisha ni kusonga mbele pia jifunze kutokana na makosa.

  1. Tambua mambo ya muhimu ya kuyafanyia kazi

ni muhimu kuyachagua mambo ambayo ni muhimu na ya lazima katika maisha yako na  kuyatekeleza.

  1. Kuwa mtu wa kujiwekea malengo kila wakati na kujitathmini

Jiwekee Malengo kila mara na kujitathmini.Malengo yanaweza kuwa ya muda mrefu au mfupi ili kufanya Tathmini sahihi kama umeyafikia au la. Hakikikisha kwamba malengo hayo yanakuwa ni dira ya maisha yako ya kila siku.

Nakutakia Mwaka mpya wenye neema na mafanikio.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni