Makala Maalumu

Mahakama,Polisi watajwa kuwa Vinara wa Rushwa

Tarehe April 28, 2018

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) Mkoa wa Temeke imetaja Mahakama, Polisi na Sekta Binafsi kuongoza kwa kulalamikiwa zaidi kwa vitendo vya rushwa dhidi ya wananchi.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Takukuru Temeke Bi. Pilly Mwakasege ambapo amebainisha kuwa  taarifa hizo ni za kipindi cha mwezi Oktoba mwaka 2017 hadi  Machi  2018.

Amesema Halmashauri ya Manispaa ya Temeke imekuwa na malalamiko 87, Mahakama 37 na Malalamiko 26 ni ya Jeshi la Polisi ambapo malalamiko yote yameshughulikiwa na kesi kupelekwa Mahakamani.

Ameongeza kuwa  Takukuru imeweza kuokoa zaidi ya shilingi milioni 44 kutoka kwa mishahara hewa, mfuko wa jimbo, malipo ya zabuni kwani wanasimamia fedha zote za miradi ya maendeleo na kuwahimiza Wananchi kuendeleza ushirikiano na mamlaka hiyo katika kudhibiti vitendo vya rushwa

Kuhusu kutoa Elimu Mwakasege amesema lego la kuwaelimisha Wananchi Juu ya Haki na Wajibu wao katika kupambana na rushwa, kuwaelewesha njia za kuwasilisha malalamiko na kutoa elimu ya uelewa wa masuala ya rushwa.

 

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni