Makala Maalumu

MAENDENDELEO YA VITU  NI MAENDELEO YA WATU

Tarehe May 8, 2018

Saidi Nguya

*Leo ninawaletea makala fupi  yenye kufafanua maendeleo yanayafanywa na serikali ya awamu ya tano yenye kuhusisha vitu na namna yanavyoweza kuathiri maendeleo ya watu.

Kumeibuka mijadala mbalimbali inayohusiana na maendeleo yanayofanywa na serikali katika kipindi hichi na wengine wakihitimisha kwa kutokukuonesha uhusiano uliopo kati ya vitu na watu.

Kwanza kabisa ningependa ifahamike kuwa, hatua yoyote ili iitwe maendeleo ni lazima ihusianishe na iwe na muelekeo wa upatikanaji wa riziki kwa watu, urahisishwaji wa shughuli za watu na ihusike katika ulinzi na usalama wa watu.

Mara kadhaa Ndg John Joseph Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani amekuwa akisistiza kwa kurudia kuwa, “Tunataka Tanzania iwe nchi ya mfano, tumechoka kusindikiza, tunataka wengine watusindikize”. Hii ni kauli na imekuwa ikitimilika kwa hatua mbalimbali lakini hatua ya mwisho kabisa ni kuifanya Tanzania kuwa Nchi ya Viwanda.

Tanzania si Nchi ya kwanza wala haitakuwa ya mwisho kuwa na uchu wa uchumi wa viwanda. Katika dunia ya sasa ambayo kwa kiasi kikubwa kumekuwa na ushindani mkubwa unaopelekea urafiki w mashaka baina ya mataifa mbalimbali ni wakati muafaka kujijenga kuwa na uchumi thabiti usikuwa na chembe ya utegemezi katika mambo ya msingi.

Katika nchi za dunia ya kwanza na ambazo zimefikia hatua ya kuitwa Dunia ya kwanza miongo michache iliyopita kwa ukuaji wa uchumi zilifanikiwa kwa kiasi kikubwa kupitia Viwanda. Nchi hizo ni China, Taiwan, Indonesia pamoja na Jamhuri ya watu wa Korea ( kusini na kaskazini).

Katika kitabu cha bwana Matleen Kniivila kiitwacho “Industrial development and economic growth: Implications for poverty reduction and Income Inequality. Ameeleza namna maendeleo ya vitu ikiwemo viwanda vinavyoweza kuinua maendeleo ya watu akitolea mfano katika nchi za China, Taiwan, India na Korea

Baada ya vita kuu ya pili ya Dunia, China ilichukua hatua za maendeleo kadhaa ikiwemo ukuzaji na uimarishaji wa uchumi wa viwanda ambapo mazao mbalimbali ya kilimo yaliyozalishwa kupitia sera yao ya kilimo ya Mapinduzi ya Kijani, mazao yalisafirishwa moja kwa moja viwandani tayari kwa kuchakatwa na kutengeneza bidhaa mbalimbali, ikiwemo nguo, viatu, bidhaa za chakula n.k.

Kutokana na hatua hiyo ya kuelekea katika uchumi wa viwanda iliyoshamirishwa na mapinduzi ya kilimo,  katika miaka ya 1980 na 1990 GDP iliongezeka zaidi na kufikia kuwa ni nchi ya kwanza katika ukuaji wa uchumi kwa kufikia 9.9 hadi 10.3 kutoka 6 GDP ya awali katika miaka ya 1970 mwanzoni takwimu kutoka benki ya Dunia.

Katika kitabu hicho cha bwana Matleena Kniivla anaeleza kuwa, ukuaji mkubwa na waharaka wa uchumi umetokana na jitihada za dhati katika maendeleo ya viwanda, iliyopelekewa na uimarishaji wa nishati ya umeme, ujenzi wa miundombinu, udhibiti wa masoko ya ndani na upatikaji wa wafanyakazi.

Maendeleo hayo ya vitu ndio yaliyopelekea maendeleo ya watu yakakua kwa kiasi kikubwa kwa upatikanaji wa ajira kwa urahisi ikijumuisha wenye taaluma na wasio na taaluma, pia imepelekea upatikanaji wa fedha za kigeni kwa maana fedha nyingi zilizokuwa zikitumika kuagiza bidhaa kutoka nje zilitumika kufanya maendeleo ya watu ikiwemo  mishahara ya watumishi kuongezwa na kusajihisha kiwango na uchangamfu wa biashara katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Ikumbukwe kuwa ifikapo mwaka 2025 Tanzania itakuwa imeondolea katika nchi masikini katika mpango wa maendelo wa Dunia hivyo kukosa misaada mingi tunayoipata katika kipindi hichi, hivyo Tanzania katika kipindi hichi na serikali hii ya awamu ya Tano, imejikita katika Mapinduzi ya Viwanda ambayo yameenda sambamba na ujenzi wa miradi mikubwa ya umeme ili kuongeza Nishati viwandani. Moja ya miradi hiyo ni ule mradi wa Kinyerezi I – unaotarajiwa kuzalisha MW 325 tofauti na sasa MW 150 na unagharimu shilingi bilioni 400.
Hivyo hivyo ujenzi wa Kinyerezi II unakadiriwa kutoa umeme MW 240 na asilimia karibia 20 za gharam ya mradi zinalipwa na Serikali ya Tanzania.
Lakini pia kuna kinyerezi III MW 600, na Kinyerezi IV umeme MW 330.

Mbali na miradi ya kinyerezi kuna miradi mingine ya Somafunga unatarajiwa kuzalisha umeme wa MW 330 karibia na ule mradi wa Mtwara utakaozalisha umeme MW 300. Zaidi ni mradi mkubwa kabisa wa uzalisha wa umeme ambapo mchakato wake ulianzishwa na baba wa taifa Mwl. JK Nyerere unaitwa Mradi wa Stigler’s gorge unaotarajiwa kuzalisha umeme wa  MW 2100 huku ukigharimu fedha za ndani shilingi Tirioni 3.

Lakini pia katika upande wa miundombinu Serikali hii ya awamu ya tano, mbali na mtandao wa barabara unaoendeleo kutapakaa nchi nzima na ujenzi wa vivuko na ununuzi wa meli kubwa za kisasa katika maziwa ya Tanganyika, Viktoria, Nyasa.  Imeanza ujenzi wa reli ya kisasa ( Standard gauge Railway ) ya kihistoria inayoanzia Dar Es Salaam na kupita Mikoa ya Morogoro, Dodoma, Singida, Tabora, na kuelekea Mwanza na Kigoma. Reli hii ndio Reli bora zaidi Afrika mashariki na kati yenye uwezo wa kupitisha Treni itumiayo umeme na mafuta na mwendokasi wa Km 160 kwa saa huku ikivuta mabehewa yenye uzito wa tani elfu 30 sawa na Semitrela 500 kwa safari moja. Ujenzi huu unagharimu zaidi ya shilingi tirioni moja na kwa kiasi kikubwa ni fedha za ndani.

Viwanda hutegemea nishati ya umeme, viwanda hutegemea Miundombinu thabiti ya reli, maji, barabara na anga ili kuweza kusafirisha malighafi kuelekea viwandani na bidhaa kutoka viwandani kuelekea kwa watumiaji ndani ya nchi na nje ya nchi. Hii haina tofauti na namna maendeleo ya viwanda yalivyofanyika katika nchi za China, india, Korea, Taiwani n.k ambapo baada ya muda maendeleo ya watu yaliibuka kwa kasi kutokana na uwepo wa ajira za kudumu na za muda viwandani na Nchi kupunguza matumizi ya fedha za kigeni katika manunuzi ya bidhaa za nje na kufanya kuwa na fedha za kigeni za kutosha na uchumi kukua kwa haraka zaidi.

Lakini pia kitabu cha Mwl Julius Nyerere cha “Tanzania ten years after independence” mwalimu anasema “this industrial development has an effect on the whole economy, it creates employment for tanzanians and the money which is spent on these goods circulates within the country – the workers buys food, clothes and other things from his wages thus providing still more employment and stimulating other activity. At the same time we are saving the foreign exchange, Hence development of industries is the development of people”. Kwa tafsiri isiyo rasmi, maendeleo ya viwanda yanaatahari chanya katika uchumi, yanatengeneza ajira, na yanafanya mzunguko wa fedha wa ndani kuwa na tija kwa kusaidia kuhifadhi fedha za kigeni kwa kiasi kikubwa, hivyo maendeleo ya viwanda ni maendeleo ya watu.

Anachokifanya Rais John pombe Magufuli ndicho walichokifanya viongozi mbalimbali wa mataifa yalioendelea na hali tunayoipitia sasa ni sawa na hali walioipitia wananchi wa mataifa mbalimbali yalioendelea. Uvumilivu wao, na mshikamamo wao, ndio sababu kubwa ya hapo walipo sasa.

Tanzania tunaweza.
Watanzania tunaweza
Magufuli anaweza
Tuungane kuilekea Tanzania mpya.

Na mwandishi wenu

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni