Makala Maalumu

Fahamu mambo kadhaa kuhusu Krismasi

Tarehe December 22, 2016

Ornaments on a Christmas tree

Ni rahisi sana kupotelea katika kufurahia zawadi na idadi ya mishumaa katika Sikukuu ya Krismasi lakini ukweli ni kuwa kwa hivi karibuni Krismasi imekuwa siku kubwa sana inayochukua sehemu kubwa ya mapumziko yetu. Pengine jambo la kwanza la kujiuliza, ni kwanini tunasherehekea sikukuu hii?

Kuna wakati huko nyuma ambapo Wakristo walikuwa hawasherekei siku zao za kuzaliwa, achilia mbali ya Kristo mwenyewe, wakiamini kuwa sherehe za kuzaliwa ni kama mambo ya ‘kipagani’ zaidi, hivyo kuna mengi sana ambayo hatuyajui, ama tumesahahu ya jinsi gani Krismasi ya kisasa ilivyokuja kuwa ilivyo sasa.

Illuminated christmas tree on the snow at night

Kwanini tunasherekea Sikukuu ya Krismasi Desemba 25

Sikukuu ya Krismasi inasherekea historia ya mzaliwa, lakini Biblia haionyeshi uhusiano wa Kristo kuzaliwa mwezi Desemba.  Wasomi wanaamini kuwa kuna uwezekano mkubwa Yesu alizaliwa majira ya joto ‘spring’ (Kwa mujibu wa Kitabu cha Luka anasema kulikuwa na wachungaji nyikani katika Krismasi ya kwanza, kitu ambacho kinaonyesha haikuwa wakati wa baridi).

Baadhi ya watu pia wanaamini kuwa Desemba 25 iliibuka kama mbadala wa Wakristo kwa Wapagani wa Kirumi ambao walikuwa wakisherekea siku hiyo katika majira ya baridi, na hivyo kuamua kuifanya Desemba 25 kama siku ya kusherekea siku hiyo.

Wengine wanafikiri siku hiyo itakuwa imepatikana baada ya kupiga mahesabu toka siku ya kudhaniwa ya kusulubiwa Yesu ya April 6 ikiambatana na imani kuwa manabii/mitume walikufa siku hiyohiyo ya kwa mujibu wa ubunifu wao.

A young boy dressed in Santa pajamas places a star a top the Christmas tree.

Utamaduni wa mti wa Krismasi umetokea wapi

Warumi wa Kipagani kwa muda mrefu sana hawakuwa  wamepamba nyumba zao kwa vitu vya rangi ya kijani kuwakilisha mzunguko wa maisha ambao ulikuwa unadumu katika miezi ya baridi. Kufikia miaka 1500 mti rangi ya kijani ukaibuka kama alama ya Krismasi huko Latvia na Stasbourg. Wengine wanaitaja ujerumani kama nyumbani halisi kwa mti wa Krismasi ulipoanzia. Tamaduni hiyo ilisambaa katika makoloni ya Marekani katika karne ya 18 na kufuatia ujio wa wahamiaji kutoka Ulaya katika maeneo kadhaa duniani ikiwemo barani Afrika na hadi leo tunatumia mti maalum wa kijani kama alama ya Krismasi.

Matumizi ya Xmas kama kifupisho cha Christmas ni sahihi?

Matumizi ya kifupisho cha Krismasi, ‘Xmas’ yamekuwa yakiibua maswali kama ni sahihi ama sio sahihi, lakini matumizi ya kifupisho hicho ni sahihi kwa mujibu wa elimu ya dini (theologically). Neno la Kigiriki X au Chi, ni herufi ya kwanza ya neno ‘Christ’ yaani Yesu. Christmas ilijulikana kama “Xtemmas,” na baadae ikafupishwa kuwa “Xmas”.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni