Makala Maalumu

Biashara 5 zitakazokupa uhakika wa soko katika uchumi uliodorora

Tarehe April 1, 2018

Soko la Kariakoo jijini Dar es salaam.

Watu wengi wamekua wakiwaza ni kwa namna gani wataweza kufanya biashara ambayo inawapa faida katika uchumi uliodorola ambayo baadhi ya wafanyabishara wameshindwa kuhimili na kufunga biashara zao.

Ili kukabiliana na hali ya ngumu ya kiuchumi zipo biashara ambazo unaweza kufanya na zikakufanya upate faida  na kuhimili uchumi uliodorola.

Biashara hizo ni zile ambao zipo katika  kundi la huduma ambazo hata kukiwa na hali mbaya ya kiuchumi ni lazima watu watanunua.

Hizi ni baadhi ya  biashara ambazo ukifanya lazima utapata faida,.

Biashara  au  Huduma za Vyakula
Hii ni Sekta ambayo ina wateja wengi sana na ni ngumu kuyumba ata uchumi ukiyumba vipi kwa sababu kila mtu lazima ale,pia kipaumbele cha binadamu kwa kwanza ni kula.Kwa hiyo unaweza kuwekeza katika maduka ya vyakula,bidhaa za kilimo n.k.

Bishara katika Sekta ya urembo na utanashati
Duniani  kote  urembo na utanashati ni tabia ambayo si rahisi mtu  kuiacha.Watu wa rika zote huwa na tabia ya kupenda urembo na utanashati.Wanawake ndio kundi pekee ambalo  hupenda kununua vipodozi  hata kama kukiwa na hali mbaya ya kiuchumi.

Katika sekta ya urembo biashara unazoweza kufanya zimegawanyika katika makundi  kadhaa ikiwemo ya  Viatu,Vipodozi,Saloon pamoja na nguo.

Bisahara ya Pombe,vinywaji   na vilevi

Katika zama hali ngumu ya kichumi baadhi ya watu hupenda kupunguza mawazo kwa kutumia vilevi hasa pombe. Hivyo basi licha ya hali ngumu ya kichumi ila baa bado zinapata wateja kila kukicha.

Katika kundi hili unaweza kufanya bishara ya duka la vinywaji,wakala wa jumla na rejareja pamoja na kufungua baa na grosari

Sekta ya  Michezo

Sekta ya michezo ni pana sana.Katika michezo unaweza kufanya bishara ya kuonyesha mpira, kuprint tshirts, video games  na kufungua betting centre.

Sekta ya ufundi & Repairing centre.

Katika hali ngumu ya kichumi baadhi ya watu huwa hawanunui vitu vipya madukani,badala yake hupeleka kwa fundi vitu vilivyoharibika ili kuepuka gharama.

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni