Makala Maalumu

Kisa cha Gaddafi na Weifenbach, fundisho kwa soka la ushindani

Tarehe June 12, 2017

 

Kikosi cha Simba katika michuano ya Sport Pesa mwaka 2017.

Kikosi cha Simba katika michuano ya Sport Pesa mwaka 2017. Katuni la Sport Pesa likiwa pembeni ya kikosi hicho kilichotolewa katika hatua ya kwanza ya michuano hiyo iliyoanza kutimua vumbi Juni 5 na kuhitimishwa Juni 11. Bingwa wa kwanza ni Gor Mahia.

Juni 3 mwaka huu tulishuhudia Klabu ya Real Madrid ya Hispania ikiendeleza ubabe mwingine katika medani ya soka baada ya kutwaa taji la 12 la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Juventus walijitahidi kufanya wawezalo dhidi ya wababe hao wa Ulaya na dunia kwa sasa lakini waliishia kutandikwa mabao 4-1.

Kilichovutia kwa mara nyingine katika dimba la Cardiff, mbele ya watazamaji zaidi ya 70,000 raia wa Ureno Cristiano Ronaldo alipochukua kiatu kwa mara nyingine akiongeza mbao mawili aliyoyafunga wakati wa fainali hiyo yalimpa ujiko kocha Zinedine Zidane.

Hakika rekodi ya kulitetea taji la Ulaya sio kazi ya mchezo mchezo inahitaji moyo wa kiongozi wa zamani wa Libya aliyeuawa kikatili nchini mwake sio mwingine ni Kanali Gaddafi.

 

Colonel Muammar Gaddafi

Colonel Muammar Gaddafi

Mei 7, 1942 alizaliwa kiongozi huyo wa zamani wa Libya Kanali Muammar Gaddafi. Jina lake halisi ni Muammar Mohammed Abu Minyar Gaddafi. Alizaliwa katika mji wa Sirte katika familia maskini. Alifariki dunia Oktoba 20, 2011 baada ya mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.

Gaddafi ambaye alichukulia umaarufu mkubwa alikalia uongozi wa taifa hilo kuanzia mwaka 1977 hadi kifo chake. Alianza kuwa mwanaharakati tangu alipokuwa shuleni Sabha na baadaye alifanikiwa kuingia jeshini mjini Benghazi.

Baada ya mapinduzi ya mwaka 1969 aliingiza Libya katika mfumo wa Jamhuri akiwaondoa Waitaliano na misingi yote ya Kimagharibi na kujikita kujenga taifa lakeakiwa karibu sana na Misri wakati huo ilipokuwa mikononi mwa Gamal Abdel Nasser.

‘The Green Book’ ndicho kilichompa umaarufu mkubwa mwanasiasa huyo.  Hata hivyo kuna mengi ambayo yanaweza kutajwa kwa Gaddafi lakini kuna jambo moja ambalo huwa halipewi uzito wa juu. Jambo hilo ni hili, ‘Je, Kanali Gaddafi alikuwa mpenda michezo?’ au ‘Aliipa nafasi kiasi gani michezo katika taifa lake?. Tuangazie hapo katika maktaba yetu ya leo.

Mchezo wa Magongo katika barafu (Ice Hockey) sio maarufu sana kwa nchi nyingi zilizoko katika ukanda wa joto hapa ulimwenguni ikiwamo Tanzania. Hapo ndipo unaweza kumshangaa Kanali Gaddafi kujiingiza katika mchezo huo licha ya kwamba aliingia kwenye soka.

Ice Hockey imekuwa maarufu sana Amerika ya Kaskazini hususani katika nchi ya Marekani na Kanada kutokana na kuwa na mazingira yanayoweza kuufanya mchezo huo ukachezeka. Pia kuna nchi nyingine barani Ulaya kama Ujerumani zimekuwa zikiucheza sana mchezo huo.

Klabu za Ulaya zilikuwa zikisajili wachezaji kutoka ligi ya Ice Hockey ya Marekani (NHL) ili kuongeza nguvu katika vikosi vyao. Wachezaji kama Auston Matthews kutoka Arizona nchini Marekani walitimkia Uswisi kucheza mchezo huo.

Kwa muda mrefu Ulaya imekuwa sehemu nzuri kwa wachezaji kutoka  Amerika ya Kaskazini kucheza mchezo huo. Lakini kuna wachezaji wawili kutoka Canada Dan Olsen na Bruce Hardy waliofanikiwa kucheza Ulaya hususani nchini Ujerumani. Huko walitua katika klabu ya Iserlohn iliyokuwa na maskani yake Kusini mwa Dortmund.

Waliwahi kuhojiwa  na vyombo vya habari kuhusu maisha yao walipokuwa katika ardhi hiyo. Hardy  alisimulia kisa kimoja katika klabu ya ECD Iserlohn waliyokuwa wanaitumikia. Kisa hicho kilikuwa ni udhamini wa Kanali Muammar Gaddafi.

Hiyo ilikuwa mwaka 1987 wakati wakihudumu chini ya mmiliki wa Heinz Weifenbach ambaye hakika aliupenda mchezo wa Ice Hockey na klabu ya Iserlohn. Hakupenda kuona wachezaji wakipata shida, wakishindwa kupata stahili zao, hakupenda kuona klabu ikifilisika.

Mchezo ukididimia nchini humo.  Hardy alisema udhamini wa wachezaji na  timu katika Ice Hockey ya Ulaya ilikuwa ya kustaajabisha sana kwani waliokuwa wakipata udhamini hususani wachezaji walikuwa wakitambuliwa kwa helmet zenye rangi ya dhahabu yaani kwa ufupi vifaa vizuri.

Hardy alisema  Weifenbach ambaye alikuwa mmiliki wa Iserlohn ni mtu sahihi ambaye dunia ilikuwa inamhitaji. Aliweka utajiri wake ili kuifanya timu hiyo kuwa miongoni mwa timu bora na za juu. Olsen naye aliyakumbuka maisha ya mmiliki huyo kuwa hakuwa mwoga kwa wachezaji kujua alichokuwa akifikiria katika mchezo huo.

Olsen alisema kuna wakati alikuwa akiingia katika vyumba vya kubadilishia na wakati mwingine timu inapofanya vibaya alikuwa akiapa kuondoka Ujerumani zaidi sanakuna siku alishawahi kutoa bastola yake kutoka viunoni mwake. Kwa staili hiyo alitengeneza kikosi imara na kigumu.

Hardy alimwezea Weifenbach kuwa ni miongoni mwa watu wa kustaajabisha aliowahi kukutana nao. Sasa ilifika wakati klabu hiyo ya Ujerumani ilikuwa kwenye wakati mgumu kiuchumi ikidaiwa kodi na mamlaka za nchini humo kiasi cha dola milioni 3.4  hali iliyosababisha klabu kushindwa kucheza, kulipa mishahara ilikuwa taabu, wachezaji kushindwa kufanya mazoezi na makocha kuja na kuondoka kutokana na kukosa mishahara.

Mhasibu wa klabu hiyo wakati huo ‘Merlin the Magician’ alikuwa kwenye wakati mgumu pia katika mamlaka za nchi hiyo. Weifenbach hakukubali aliamua kukwea pipa hadi nchini Libya kukutana na Kanali Gaddafi ili aweze kuwa mwekezaji katikaIserlohn. Gaddafi alikubali kumpa dola za Marekani 900,000 ili kuinusuru klabu hiyo.

Lakini Kanali Gaddafi alimpa kwa masharti kuwa katika jezi za Iserlohn kungekuwepo alama ya kitabu chake cha ‘The Green Book’. Hakuana aliyeshangaa kuona Gaddafi anakubali dili hilo lakini kwa wafuatiliaji wa masuala ya kiuchumi, Libya ilikuwa mshirika mkuu wa Ujerumani kutokana na malighafi ya mafuta kwa muda mrefu.

Kilichokuja kuharibu ni lile shambulio la Lockerbie Desemba 21, 1988 pale Pan Am Flight 103 ilipoanguka na kuua abiria 243 na wafanyakazi 16 wa ndege hiyo katika eneo ka Lockerbie, Scotland. Kanali Gaddafi alikuwa akirushiwa lawama kuwa alihusika katika shambulio hali iliyozua jambo.

Pia Gaddafi alitupiwa lawama kuwa alihusika kuwaua watu watatu na wengine 230 katika ukumbi wa disco wa La Belle ambako Askari wawili wa Marekani waliuawa na Wamarekani wengine 79 kujeruhiwa. Sasa wakati Weifenbach alipokubali kuweka udhamini mbele ya jezi za klabu yake alichukuliwa kuwa msaliti anaunga mkono sera za mbaya wao hali iliyowatishia kudidimiza klabu yake.

Shirikisho la Ice Hockey la Ujerumani lilikaririwa na Der Spiegel kuwa Weifenbach anachukuliwa kuwa Sodoma na Gomora pia Waziri wa Mambo ya Ndani Friedrich Zimmermann naye alipigilia msumari. Pia kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani ya mchezo huo wakati huo Xavier Usinn alikaririwa akisema wachezaji wa kigeni hawapaswi kuchukuliwa kuwa wanajihusisha na makosa ya jinai na ugaidi.

Juma lililofuata timu ya Iserlohn ilikuwa na mchezo ugenini jijini Frankfurt ambako badala ya kupokewa kwa shangwe na bashasha walipokewa na waandamanaji na polisi katika uwanja waliokuwa wanaenda kucheza mechi. Hardy alisema kuwa wachezaji waligundua ni kwasababu ya udhamini wa Kanali Gaddafi sasa iliwabidi wachukue msimamo mkali katika suala hilo.

Kucheza na jezi za zamani au mpya zenye nembo ya Green Book. Katika hilokulikuwa na sura mbili waamue kuizamisha klabu ipotelee mbali au wakubali kukosolewa na vyombo vya habari ili klabu ipone isifilisike. Wachezaji waliamua kucheza kwa kuvaa jezi za zamani.

Weifenbach aliingia katika vyumba vya kubadilishia na kuwaambia kuwa anaheshimu mawazo na uamuzi wao na kwamba mchezo huo ungekuwa wa mwisho kwa timu hiyo kwani klabu haitakuwa na uwezo wa kujiendesha bila fedha kutoka kwa wadhamini.

Hata kama angewalazimisha wachezaji kuvaa udhamini wa ‘Green Book’ bado angefungiwa na shirikisho la mchezo huo nchini Ujerumani. Gaddafi hakuamini lililotokea baada ya kupokea taarifa hizo. Weifenbach aliachana na uendeshaji wa klabu hiyo na kurudi zake.

Hardy naye akirudi zake Alberta baada ya kucheza zaidi ya miaka 10 nchini Ujerumani, lakini akiwa na jezi ya Iserlohn iliyokuwa na nembo ya udhamini ya Green Book. Weifenbach alifariki dunia Februari 21, 2015 akiwa na miaka 75.

Jezi ya udhamini wa Gaddafi imehifadhiwa kwenye makumbusho ya Ujerumani kamakumbukumbu na kutambua mchango wa Weifenbach katika hockey. Licha ya Gaddafi kujihusisha na Ice Hockey lakini enzi zake alishawahi kutoa fedha katika klabu za kandanda za Perugia na Sampdoria za Italia ili ziweze kujiendesha. Hakika Kanali Gaddafi atakumbukwa na wengi duniani kote kutokana na ujasiri katika kile alichokuwa akiamini.

Sport Pesa Cartoon

Sport Pesa Cartoon

Michuano ya Sport Pesa imeanza Juni 5 na kuhitimishwa Juni 11 mwaka huu katika dimba la Uhuru jijini Dar es Salaam. Katika michuano hiyo kumeshuhudiwa timu kutoka Tanzania, Singida United, Yanga, Simba na Jang’ombe Boys zikipambana dhidi ya zile za Kenya AFC Leopards, Tusker FC, Nakuru All Stars.

Hatimaye Bingwa wa michuano hiyo amejulikana kuwa ni Gor Mahia. Hapo sihitaji kuzungumza mengi. Katika michuano hii kuna mambo kadha wa kadha yanapaswa kuwa fundisho kwa klabu zetu, ili zipate kujiendesha kiuchumi. Lakini leo nizungumze kuhusu ‘Katuni ya Sport Pesa’

Kuna klabu yoyote ambayo imeona ubunifu huo ambao klabu nyingi barani Ulaya zimekuwa na midoli ya jinsi hiyo inayotambulisha klabu zao.

Hapa nchini midoli hiyo imekuwa ikitengenezwa na mashabiki na wapenzi kwa binafsiyao hali ambayo hata viongozi wa klabu husika hawalioni hilo wanao ni kawaida tu.

Mosi inafungua ajili kwa anayekuwa katika mavazi ya jinsi hiyo hivyo kama kuna watu nyuma ambao wanamtegemea basi hawataacha kuipenda klabu hiyo kwasababu inawapa riziki.

Tumekuwa na dhana potofu kuwa riziki inatoka kwa Mungu, misemo kibao kama ipo ipo tu na mingine mingi. Lakini tumekuwa tukijibweteka bila kupambana kutafuta fursa na kusalia kuwa na ndoto ambazo hazitimiziki.

Kanali Gaddafi aliona fursa akaitumia hata kama haikutimia lakini alithubutu kufanya kwa Iserlohn hadi sasa ni alama, hata Ujerumani wanatambua mchango wa Gaddafi katika maendeleo ya michezo nchini mwao.

Imetayarishwa na Jabir Johnson

Email this page

To:
From
Subject
Message
Code

Maoni